Treni mpya ya abiria yenye kufanya safari zake kati ya Dar es Salaam na mikoa ya Kigoma na Mwanza, ikiwa kwenye kituo kikuu cha reli (TRL), jijini Dar es Salaam leo Jumatano Aprili 1, 2015. Treni hiyo iliyopewa jina "Deluxe Coach" imezindua safari yake ya kwanza leo Aprili mosi, kuelekea Kigoma, ikiwa na mabehewa mapya yaliyoagizwa na serikali hivi karibuni. Injini zilizokarabatiwa na wamalaysia, zimeonekama kama mpya na sasa treni hiyo itakuwa ikisafiri kila Jumapili saa 2 usiku ikitumia masaa 30, ambayo ni pungufu ya masaa 6 yanayotumiwa na treni ile ya kawaida. Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa TRL, Kipallo Aman Kisamfu aliiambia K-VIS blogu kuwa treni hiyo haitakuwa na vituo vingi na kutaja kuwa iking'oa nanga Dar es Salaam, kituo cha kwanza ni Morogoro, na kufuatiwa na Kilosa. Baada ya hapo itasimama kwenye stesheni ambazo ziko Wilayani na mikoani. Treni hiyo itakuwa na madaraja ya tatu ambayo hutumiwa na "makabwela", daraja la pili kukaa, daraja la pili kulala, daraja la kwanza na pia patakuwa na hoteli ya kisasa kabisa. treni hiyo mpya inazo huduma za maji kwenye vyumba na vyoo. Meneja mkuu huyo wa TRL ametoa wito kwa watumiaji, kwa kusema neno moja tu "Tukitunze"
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Rais wa kufuatilia miradi ya serikali (PDB), Omar Issa (kulia), akizungumza na meneja mkuu Kisamfu
Meneja Mkuu Kisamfu, akikagua behewa la daraja la pili kukaa (Second Seat)
Hivi ni viti vya daraja la tatu, ambavyo abiria waliozungumza na K-VIS wamevikosoa kuwa havikuundwa kwa abiria anayesafiri safari ndefu kama ya Dar-Kigoma, bali ni safari fupi za Posta -Ubungo, kwani viko wima na hakuna namna yoyote abiria anaweza kujinyoosha kidogo kwa uchovu. "Changamoto" hiyo kwa TRL
Moja ya vyumba vya daraja la pili
Sehemu ya kuosha mikono, ambayo iko kwenye korido kwa abiria kunawa
Picha kwa hisani ya K-VIS Blog
1 comment:
Hii ndio Treni ya Kasi ???? hahahahahahahahaha wabongo tunajua kudanganyika
Post a Comment