picha hii ya maktaba inawaonyesha wavuvi wakirejea pwani baada ya shughuli ya kuvua samaki, inaelezwa kwamba wavuvi wadogo kama hawa wakiwezeshwa siyo tu wanajiongezea kipato chao lakini pia inawasidia katika utunzaji wa mazingira ya bahari .
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo akibadilishana mawazo na Balozi Manongi, mshiriki huyu kutoka Norway katika maelezo yake amesema anafanya kazi kwa karibu na serikali ya Tanzania
Pichani ni sehemu ya washiriki wa mkutano huo wa pembezoni
Balozi Manongi akibadilishna mawazo na Dr. Alf Hakon Hoel ambaye ni mtaalamu wa masuala ya utaifiti na ambaye alieleza kwamba Norway iko katika maandalizi ya mwisho ya kukamilisha meli mpya na ya kisasa zaidi ya utafiti itakayoanza kazi mwakani.
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akizungumza wakati wa mkutano wapembezoni kuhusu masuala ya uvuvi endelevu, katika mchango wake, Balozi ameeleza kuridhwa kwa Tanzania namna ambavyo wadau mbalimbali wamekuji wakijitokeza kusaidia sekta ya uvuvi na wavuvi nchini Tanzania
Hapa Balozi akibadilishana mawazo na Dr. Gabriella Bianchi ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya utafiti wa samaki, Dr Gabriella na Dr, Hoel wamefanya kazi kwa karibu sana na wataalamu wa Tanzania katika kuendeleza sekta ya uvuvi.
Na Mwandishi Maalum,
New York
Tanzania, kupitia Mwakilishi wake wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, imeelezea
kuridhishwa kwake na namna ambavyo
Mashirika ya Kimataifa naTaasisi binafsi zinavyoshirikiana na kwa karibu
na serikali na taasisi zake kuimarisha sekta ya uvuvi.
Ushirikiano huo umeifanya sekta ya uvuvi nchini kuwa wenye
tija na hivyo kuchangia katika ongezeko la kupato na kuwaondoa katika umaskini
jamii ya watanzania ambao maisha yao ya
kila siku yanategemea sana uvuvi, na pia kuimarisha utuzaji wa mazingira ya pwani na viumbe hai.
Balozi Tuvako Manongi ameyasema hayo wakati
wa mkutano wa pembezoni ( side event) uliokuwa umeandaliwa na Mpango wa
Chakula Dunia ( FAO). Mkutano huo umefanyika sambamba na mkutano usio rasmi ambapo nchi wanachama wa Umoja wa
Mataifa, wakutana ana kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya bahari na uwiano
wake katika utekelezaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu baada ya 2015.
Balozi Manongi alikuwa mmoja wa wazungumzaji
katika mkutano huo ambapo majadiliano
yalilenga zaidi katika suala zima
la uwezeshwaji wa wataalamu wa sekta ya
uvuvi na wavuvi wadogo
na wakati kwa kuwapatia mbinu na maarifa
ya kisasa ya uvuvi endelevu na unaozigatia utuzaji wa mazingira ya
bahari na viumbe hai.
Katika mchango wake, Balozi ameeleza kuwa uchumi na ustawi wa wavuvi
wengi wanaoishi pembezoni mwa bahari (pwani) nchini tanzania unategemea sana shughuli za uvuvi na kutoka
na ukweli huo, Serikali ya Tanzania, licha ya kukaribisha wabia katika kuiendeleza
sekta ya uvivu pia inawashukuru wale wote ambao hadi sasa wametoa mchango wao wa hali na mali
katika eneo hilo.
Akaongeza kuwa mafunzo na utaalamu ambao wadau
hao wamekuwa wakiwapatia wataalam wa kitanzania
kwa kuwashirikisha pia wavuvi ambao ndio wahusika wakuu, umesaidia sana katika kuwainua kiuchumi
lakini pia kuwapatia mbinu endelevu za
uvuvi na utunzaji wa mazingira.
Wadau
ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kusaidia maendeleo endelevu ya sekta ya Uvuvi ikiwamo misaada ya kiufundi ni FAO na
EAF- Nansen Project ya Norway.
Tanzania ni kati ya
nchi 32 ambazo zinashirikiana kwa
karibu na EAF –Nansen Project katika
miradi mbalimbali inayohusu uwezeshwaji wa wavuvi wadogo na
wakati. Aidha Tanzania ni kati ya nchi 10 za mwanzo zilizochaguliwa kutekeleza mpango huo.
Amesema Balozi Manongi, uvuvi
endelevu na matumizi salama ya Bahari
ni moja ya
ajenda za Malengo Mpya ya Maendeleo
Endelevu baada ya 2015 (SDGs). Ajenda
ambayo kwayo
inasisitiza usimamizi
endelevu na ulinzi wa bahari na mazingira ya pwani na
viumbe hai ili kuepusha athari mbalibmali.
Vile vile ajenda hiyo ambayo ni namba 14 inasisitiza pia uwepo kwa kanuni
bora zinazosimamia uvuvi ikiwa ni pamoja na
kudhibiti uvuvi wa kupita kiasi na uvuvi haramu, na
utoaji wa huduma za kisasa kwa wavuvi wadogo na fursa za masoko.
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzani katika Umoja
wa Mataifa ameeleza zaidi kwamba, zao la
samaki pamoja na kuwa kuchanzo cha kipato kwa watanzania
wengine na taifa kwa ujumla, lakini
pia samaki wanachangia katika kuwapatia lishe bora
watanzania na kwa sababu hiyo matumizi endelevu ya mazao ya bahari na bahari ni jambo muhimu sana.
Katika majadiliano hayo, Dr. Gabriella Bianchi ambaye ni mtaalamu wa
masuala ya utafiti wa samaki kutoka ofisi za FAO yeye katika mchango wake,
ameelezea baadhi ya mambo ambayo
wanatarajia kuyafanya katika kuzisaidia nchi za Afrika Mashariki
Tanzania ikiwamo na kwingineko Afrika
katika masuala ya usimamizi, mafunzo na utaalamu zaidi kwenye masuala ya samaki na bahari kwa ujumla.
Akasema mabadiliko ya tabia nchi, shughuli za
utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi, na uchafuzi wa bahari
ni baadhi ya changamoto ambazo wataalamu na watafiri wa masuala ya bahari na viumbe hai wa baharini kuamua kupanua wigo wa kazi zao za utafiti ikiwa ni
pamoja na mafunzo na uwezeshaji.
Naye Dr. Alf Hakon Hoel ambaye ni mkurugenzi wa
masuala ya utafiti, amesema Norway inakamilisha ujenzi wa
meli mpya na ya kisasa ya masuala ya utafiti inayotarajia kuanza
shughuli zake mwaka 2016.
Kwa mujibu wa Dr. Hoel meli hiyo itakuwa na vyumba vya
kufundishia, maabara za picha na maabara
ya tabia nchi

No comments:
Post a Comment