Na Denis Mtima / GPL
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (pichani) ametoa tamko kuhusiana na Watanzania waliopo nchini Afrika Kusini.
Waziri Membe amesema Watanzania 21 watarejeshwa nchini kutokana na vurugu zinazoendelea za wenyeji kuwashambulia wageni huko Afrika Kusini.
Aidha, Membe ameongeza kuwa Watanzania watatu wamefariki kwa maradhi lakini si kuuawa katika vurugu hizo, hivyo hakuna mtu aliyeuawa kutokana na machafuko yanayoendelea.
1 comment:
Vijana kukosa kazi ni matatizo ya Viongozi wa Africa. Viongozi wa Tanznainia wanoasilikiliza sana uongozi wa World bank and IMF kukusu marekebisho ya vyombo vya Uchumi-structural Adjustment Programs pamoja na PPP( private public partnerships); kufunga viwanda vya umma ambavyo vilijengwa kwa makusudi ya kuajiri vijana pamoja na uendelezaji wa uchumi. Uchumi wa Africa nzima utakuwa na matatizo ya vurugu kama viongozi hawafanyi marekebisho ya uendelshaji wa mali asili bila kutegemea mawazo ya viongozi wa nchi ziliendela (World Bank and IMF financial models).
Post a Comment