ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 10, 2015

WANANCHI WAWAPIGA NA KUWAJERUHI WATU WAWILI WALIOKUWA WAKIBOMOA NYUMBA ENEO LA KININDONI- MANYANYA JIJINI DAR


Watu wawili wamejeruhiwa vibaya na kunusurika kufa akiwemo askari mgambo baada ya kupata kipigo kutoka kwa wananchi wakati walipokuwa wakibomoa nyumba ya mkazi mmoja aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Husseni hali iliyosababisha jeshi la polisi kuingilia kati katika eneo la Kinondoni Manyanya jijini Dar es Salaam.
Katika tukio hilo ITV imeshuhududia kundi la watu likibomoa nyumba hiyo na kutoa vitu nje huku askari wa mgambo wakiwa wanasimamia zoezi hilo ambapo, baada ya kukamilika kwa zoezi hilo wananchi wa maeneo hayo waliwavamia baadhi ya vijana walikuwa wakibomoa nyumba hiyo na kuanza kuwashumbulia kwa mawe na zana mbalimbali bila ya kupata msaada wa kuokolewa hali iliyosababisha baadhi ya magari kuvunjwa vioo na baadhi ya wafanyabiashara kulazimika kufunga maduka.
Akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa wamiliki wa nyumba hiyo bwana Ramadhani Husseni amesema wanashangazwa na kikundi hicho kuvamia na kubomoa nyumba hiyo wakati mahakama kuu ilishatoa hukumu kwa wao wanahaki ya kumiliki nyumba hiyo kisheria. 
Kwa upande wake mmoja wa wakazi katika nyumba hiyo amelalamikia kikundi hicho kuvamia vyumba vya wapangaji kubomoa bila la kushirikisha uongozi wa serikali ya mtaa na kuiba fedha na vifaa mbalimbali.

No comments: