ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 28, 2015

Waziri Membe amuenzi Marehemu Brigedia Generali Hashim Mbita

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Bregedia Generali Hashim Mbita, kilichotokea hivi karibuni katika Hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam. Marehemu Brigedia Generali Mbita aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambabwe pia atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwenye harakati za ukombozi Barani Afrika. 
Waziri Membe akimpa pole Mjane wa Marehemu Bregedia Generali Mbita, Bi. Ngeme Mbita 
Mhe. Membe akimpa pole mtoto wa Marehemu Brigedia Generali Mbita Bi. Sheilla Mbitta 
Waziri Membe akizungumza na wafiwa 
Waziri Membe akisalimiana na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini mara baada ya kuwasili kwenye Msiba wa Brigedia Generali Hashim Mbita 
Waziri Membe akisalimiana na aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Zuberi Zitto Kabwe walipokutana kwenye msiba wa Brigenida Generali Mbita 
Waziri Membe akiwa amejumuika na Waombolezaji wengine kwenye msiba wa Brigedia Generali Mbitta nyumbani kwake Chang'ombe Jijini Dar es Salaam 
Waziri Membe akizungumza na waandishi wa Habari juu ya kifo cha Brigedia Generali Mbita. Waziri Membe alimwelezea Balozi Mbita kama kiongozi makini na mwadilifu na pia alikuwa mwanaharakati mahiri ambaye alihakikisha Bara lote la Afrika linakuwa huru. 

Picha na Reginald Philip

No comments: