ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 14, 2015

Yanga wamchanganya Msuva

Straika wa Yanga, Simon Msuva, akiwa na zawadi yake ya mchele aliyopewa na shabiki wa timu yake kutokana na jitihada zake anazofanya uwanjani. 

Msuva ambaye ni kinara wa mabao kwenye safu ya ufungaji bora baada ya kufunga 13, alizawadiwa kilo 30 za mchele wa Mbeya baada ya mechi yao na Mbeya City waliyoshinda 3-1 kumalizika. Zawadi hiyo imetolewa na shabiki maarufu wa Yanga, Ally Yanga.
MASHABIKI wa soka wanamchanganya mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva lakini mwenyewe akasema kuwa wanapomzomea au kumshangilia ndiyo wanamfanya afanye vizuri kama alivyo sasa.

Msuva ambaye ni kinara wa mabao kwenye safu ya ufungaji bora baada ya kufunga 13, alizawadiwa kilo 30 za mchele wa Mbeya baada ya mechi yao na Mbeya City waliyoshinda 3-1 kumalizika. Zawadi hiyo imetolewa na shabiki maarufu wa Yanga, Ally Yanga.

Kuhusu hilo, Msuva alisema: “Unajua wakati mwingine mashabiki huwa wananichanganya sana, kuna wakati wanakushangilia, kisha hao hao baadaye wanakuzomea, wananichanganya sana.

“Lakini naweza kusema wamenisaidia kwa kiasi kikubwa kwa sababu matukio yao ndiyo yanakufanya mchezaji utambue thamani yako kama mchezaji.

“Unajua ni kama wanakukumbusha ujijue ni kitu gani unachotakiwa kukifanya kwa wakati huo kulingana na namna wanavyokupokea, zawadi ya mchele waliyonipa nimeitoa kwa wazazi wangu waende wakale. Unajua wao ndiyo kila kitu.”

Ally Yanga alisema: “Nimempa Msuva mchele wa Mbeya, nimependa tu kwa sababu ni mchezaji ambaye naweza kusema ndiye anastahili zawadi kwa sasa kutokana na bidii yake uwanjani.”

No comments: