ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 29, 2015

ZIMBABWE YAIPA MAJENGO SADC KWA AJILI YA KITUO CHA KUFUNDISHIA WALINDA AMANI


Rais wa Zimbabwe na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Mhe. Robert Mugabe akiangalia Hati Miliki ya Majengo ambayo Serikali ya Zimbabwe imetoa kwa SADC kuwa Kituo cha Kufundishia Walinda Amani. Hati hiyo ilikabidhiwa kwa Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt. Stergomena Tax anayeonekana kushoto. Majengo hayo yapo kwenye kiwanja chenye ukubwa wa ekari 16 ambayo Zimbabwe imetoa bure kwa SADC kama mchango wake wa kuhamasisha amani na utulivu barani Afrika.

Rais Mugabe akionge machache mara baada ya kukabidhi Hati Miliki ya majengo ya Kituo cha Kufundishia Walinda Amani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal (kulia) akishuhudia Rais wa Zimbabwe akikabidhi majengo hayo kwa Katibu Mtendaji wa SADC.

No comments: