WATU zaidi ya 43 wamepoteza maisha huku wengine kadhaa wakijeruhiwa katika shambulio lililofanywa na watu wenye silaha walioshambulia basi huko Karachi, Pakistan.
Basi lililoshambuliwa na watu hao lilikuwa limewabeba waumini wa dhehebu la Shia.
Polisi wa Karachi wameeleza kuwa washambuliaji wapatao sita wakiwa katika pikipiki walilishambulia basi katika eneo la Safoora Goth kwa risasi na kuua watu hao 43.

No comments:
Post a Comment