Timu ya soka ya Arsenal usiku wa kuamkia leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Hull City katika mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza.
Mlinda mlango wa Hull City, Steve Harper akiwa hana la kufanya zaidi ya kuuangalia mpira ukijaa wavuni.
Ikicheza ugenini katika uwanja wa KC, washika bunduki hao wa jiji la London walionyesha kandanda la hali ya juu na kuonyesha ubora wao wa kumiliki mpira hadi mwisho wa mchezo wao.
Mabao mawili toka kwa mshambuliaji wake mwenye kasi Alexis Sanchez katika dakika za 28 na 45 na bao jingine toka kwa Ramsey alilofunga katika dakika ya 33 yalitosha kuipa ushindi huo na kufikisha pointi 70 sawa na Manchester City lakini wakitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.
No comments:
Post a Comment