ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 20, 2015

BALOZI AMINA SALUM ALI ATANGAZA KUWANIA URAIS


BALOZI wa kudumu wa Umoja wa Afrika (AU), huko Marekani, Mtanzania Amina Salum Ali, (Pichani) akitangazaleo Jumatano Mei 20, 2015, pale kwenye mgahawa wa Hadees jirani na askari monument, kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.

Balozi Amina ametangaza uamuzi wake huo mapema leo hapa hapa jijini Dar es Salaam.
Itakumbukwa ya kuwa Balozi Amina ambaye alidumu kwa muda mrefu kama waziri kwenye serikali ya Rais mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Salmin Amour Juma, almaarufu kama (Komandoo), aliwahi kutupa karata yake kuwania urais wa Zanzibar, kabla ya kujitoa.

Huyu anakuwa mwana mama wa kwanza kwenye historia ya chama cha Mapinduzi CCM, kutangaza kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hali kadhalika, Balozi Amina rekodi yake ya kwanza ni kuwa mwanamke wa kwanza kuwa balozi wa kudumu wa AU huko Marekani.

Mbali na kuwahi kuwa waziri, Balozi aAmina ndiyo muasisi wa taasisi ya Zanzibar Women Welfare Trust, inayojishughulisha na kupambana na afya ya akina mama na watoto hususan kwenye eneo la maambukizi ya VVU.

Kitaaluma Amina anayo shahada ya uchu
Balozi Amina akiwa na Rais Mstaafu wa Marekani, George Bush
Balzoi Amina akiteta jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu huko Marekani
Amina akiwa na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein
Amina akiwa na Waziri wa Mmabo ya Nje wa Marekani John Kerry- K-VIS Blog

1 comment:

Anonymous said...

mwandishi pia amesahau hii kuwa ni waziri wa kwanza zanzibar, wizara yake ilianzaisha na iliongoza kuwabagua wapemba ambao wote walifukuzwa kazi katika wizara ya fedha, tunampongeza pia kwa hili