ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 7, 2015

BARCELONA YAITANDIKA BAYERN MUNICH 3-0

Mlinda mlango wa Bayern Munich, Manuel Neuer akijaribu bila mafanikio kuuzia mpira uliopigwa na mshambuliaji mahiri wa FC Barcelona, Lionel Messi uliokwenda moja kwa moja nyavuni huku mabeki wake wakiwa hawana la kufanya.
Mshambuliaji wa FC Barcelona, Neymar akiifungia timu yake bao la tatu nala ushindi huku mlinda mlango wa Bayern Munich, Manuel Neuer akiwa hana ujanja. 
Wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wa Nou Camp, FC Barcelona wamewatandika wageni wao Bayern Munich jumla ya mabao 3-0 katika mchezo wa nusu fainali wa ligi ya mabingwa barani Ulaya usiku wa kuamkia leo. 

Barcelona wakicheza soka lao la kugongeana pasi za uhakika, walijipatia mabao yao kupitia kwa Lionel Messi ambaye alifunga mabao 2 katika dakika za 77 na 80 na bao la tatu likiwekwa kimiani na Neymar. 
Timu hizo zitarudiana wiki ijayo katika uwanja wa Allinz Arena. Bayern ili wafuzu kwa hatua ya fainali, itabidi wawafunge Barcelona si chini ya mabao 4-0, vinginevyo safari ndiyo inaenda kukamilishwa nyumbani kwao.

 Kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola akitoka uwanjani kichwa chini baada ya kushuhudia timu yake ikichapwa mabao 3-0 na FC Barcelona. Guardiola kabla ya kutimkia Bayern, alikuwa kocha wa FC Barcelona.

No comments: