Advertisements

Friday, May 22, 2015

Uongozi wa Ndanda FC unajipanga kukutana na bilionea namba moja barani Afrika



Bilionea Aliko Dangote

Uongozi wa Ndanda FC unajipanga kukutana na bilionea namba moja barani Afrika, Aliko Dangote kwa ajili ya kumuomba kuwa mmoja wa wadhamini wa juu katika timu hiyo kabla msimu ujao haujaanza.
Salehjembe ameripoti kwamba mwenyekiti wa Ndanda FC, Hamad Omari alisema licha ya kuwa na udhamini wa Kampuni ya Binslum na Big Tanzania, lakini wanajipanga kumuona tajiri huyo anayemiliki kiwanda cha saruji kwenye mkoa wao.

“Tunafikiria kufanya mikakati ya kuweza kukutana naye ili aweze kuwa mdhamini mkuu kwenye timu yetu ambayo imenusurika kushuka daraja.

“Unajua tangu ligi imemalizika bado hatujakaa kuweza kujadili hayo mambo na kama ataweza kukubali basi litakuwa ni jambo jema kwa sababu fedha zinazotolewa na wadhamini wa ligi hazikidhi mahitaji ya timu kwa msimu wote, sasa lazima njia nyingine zitumike kuhakikisha tunakuwa vizuri zaidi msimu ujao,” alisema Omari.


Dangote, raia wa Nigeria, kwa sasa ana kiwanda cha saruji mkoani Mtwara ambako timu hiyo inatokea, anakadiriwa kuwa na utajiri wa pauni bilioni 10.4 (shilingi trilioni 2.7) na hivi karibuni alitangaza nia ya kuinunua Klabu ya Arsenal ya England.
CREDIT:SHAFFIHDAUD

2 comments:

Anonymous said...

Watanzania tuache tamaa huyu mtu ni wakuja mnataka awe mdhamini kwa vile ni mtu nwenye pesa. Acheni tamaa hata humu tz kuna watu ambao wataweza kuwadhamini please stop doing that

Jay said...

Mkuu, una akili timamu lakini? Soma au angalia hapa duniani kuwa hili si jambo la kushangaza tena ni la kawaida. Dangote kawekeza MT, Ndanda FC inatoka MT, tatizo ni nini ikiwa makampuni makubwa ya Tanzania wao wanajali simba na Yanga tu.