Nilichokisema jana kutokana na kauli ya Mhe. LOWASSA.
Mimi nilianza kushiriki siasa toka nikiwa mdogo sana. Kuanzia Chipukizi, Greenguard wa UVCCM na baadaye UVCCM. Miaka ya mwanzo ya 90 nilivutiwa sana na mijadala ya mfumo wa vyama vingi ama kimoja. Nakumbuka, binafsi nilivutiwa zaidi na mfumo wa kutanua demokrasia, nakumbuka nilichangia hoja zangu kwenye mkutano wa tume pale Nzega mjini, viwanja vya parking pembeni ya jukwaa. Wengi kwa hakika hawakuunga mkono mfumo wa vyama vingi. Waliamini katika chama kimoja. Nilijiunga rasmi CCM mwaka 1994. Mwaka 2005, niligombea Ubunge wa Jimbo la Nzega, kura hazikutosha kwenye mchakato wa maoni ndani ya CCM na vikao vilisema kuwa wakati wangu bado.
Niliendelea kufuatilia kwa ukaribu sana kilichokuwa kinaendelea kwenye duru za siasa. Mijadala ya Bungeni ilikuwa ya moto sana, mara nyingine ikitutia simanzi sisi vijana wa CCM haswa namna tulivyokuwa tukishuhudia wabunge wachache sana wa upinzani wakiishambulia serikali yetu ya CCM kuhusiana na wimbo mpya kwenye duru za siasa za miaka hiyo, 'ufisadi'. Ufisadi ikiwa ni order of the day. Ufisadi ikiwa ni mtaji na ajenda kuu ya wapinzani Bungeni, of-course pia ajenda ya kikundi kidogo cha wabunge wa CCM waliojitambulisha kama vinara wa kupinga ufisadi. Miaka hiyo kila mtu akiuchukia ufisadi na mafisadi.
Mwaka 2008, mimi nikiwa kijana mwana mabadiliko na ninayechukia ufisadi na mafisadi, kama walivyokuwa vijana wenzangu wengi, kwenye duru za siasa na nje ya duru za siasa, nilivutiwa na mijadala iliyokuwa Bungeni kutokana na hoja iliyowasilishwa bungeni na Dr. Harrison George Mwakyembe kuhusiana na mchakato wa kununua umeme wa dharura, na zabuni hiyo kupewa kampuni ya Richmond Development Company LLC ikidaiwa kuwa mchakato huo ulikuwa na ubatilifu na mazingira ya rushwa ndani yake. Nikiwa kama mwananchi mwenye strong affinity na siasa, uongozi na namna nchi yetu inavyoendeshwa, nilivutiwa sana na namna wabunge wengi wa CCM walivyoamka na kuonesha kwa dhati ya mioyo yao namna walivyokerwa na ufisadi wa Richmond. Nakumbuka Mbunge wangu Lucas Selelii alikuwa kinara mmojawapo.
Mwanzoni sikutarajia kama Waziri Mkuu niliyempenda sana na kumuamini, niliyemtazama kama kiongozi wa mfano kwangu, aliyenivutia sana kwa namna alivyokuwa akichapa kazi na akitoa kauli za straight forward kwenye mambo mengi ya msingi, akikemea uzembe, akiadhibu wabadhirifu bila soni wala huruma, akifika kila kona ya nchi ambapo akitokea tu, basi wazembe na wabadhirifu wanaangusha angusha karatasi hovyo, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa eti naye angehusishwa kwa namna yoyote ile! Sikuamini. Lakini sikuamini zaidi niliposikia anajiuzulu...tena eti kwa sababu ya Richmond.
Nakumbuka sana kwenye duru za siasa yeye na Mjomba wangu Mhe. Jakaya Kikwete walipochukua fomu za kuwania Urais mwaka 1995, wakiwa na ujana ujana mwingi na sisi tukiwashangilia na kuwapenda kama inspirational figures wetu. Na ilipotokea mwaka 2005 alipoingia Mjomba, nilijua wazi kabisa kuwa Waziri Mkuu angekuwa Mhe. Lowassa, na tulitabiri kipindi kile kuwa Mhe. Lowassa angekuwa Rais baada ya kumaliza kipindi cha Uwaziri Mkuu, yaani 2015. Nilisimamisha kagari kangu maeneo ya Biafra na kukimbia kwenye Pub moja pale jirani kutazama televisheni iliyokuwa inarusha kutoka Bungeni, nakumbuka watu walijaa kwa wingi sana na wengi wakishangilia kuonesha kufurahishwa kwao namna serikali ilivyokuwa ikiwajibika Bungeni. Sikuamini. Serikali imeanguka! Lowassa out. Sikuamini kabisa.
Jana nikapata habari kuwa Mhe. Edward Lowassa amezungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini - amekana kuhusika kwake na Richmond. Nikashtushwa sana na hili. Nikajiuliza hivi ni nini kinataka kutokea kwenye siasa za nchi yangu? Mjadala wa Richmond ulifungwa Bungeni miaka 7 iliyopita, je inabidi ufunguliwe upya, na watu wapya tutafakari upya? Maana kuna minong'ono kuwa Mhe. Lowassa anataka kuwania Urais mwaka 2015, na ana mpango wa kutangaza nia muda si mrefu. Nikajiuliza, ni kwa nini imemchukua Mhe. Lowassa zaidi ya miaka saba kujibu hadharani kuwa hakuhusika na Richmond? Kwa nini anatamka maneno haya leo na kwa nini hakujitetea Bungeni siku ile alipojiuzulu? Nakumbuka siku ile alisema tatizo ni uWaziri Mkuu, kwa nini hakufafanua na alikuwa na fursa hiyo kama 'primus inter pares (first among equals)?' Kipindi fulani alisemekana kuwa ni 'gamba' na lingepaswa kuvuliwa...likaishia kiunoni! Ni kwa nini halikuvuka? Maswali haya sijawahi kuyapatia majibu.
Hivi ilikuwaje Rais wa Nchi, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, Kamati ya Wabunge Wote wa CCM Bungeni, na mamlaka zote za kiserikali kushindwa kumlinda Waziri Mkuu wake dhidi ya tuhuma za kuhusika kwake kwenye Richmond mwaka 2008? Maana kwenye siasa za mabunge yanayofuata mfumo wa Westminster, Waziri Mkuu ni 'primus inter pares', kwamba ana fursa ya kwanza ya kuzungumza kwenye mijadala Bungeni na ana-enjoy nguvu ya kuwa na majority bungeni kuendesha mambo ya serikali na kutawala mijadala na maamuzi. Ilikuwaje Chama kilimuacha Waziri Mkuu wake akaanguka? Ilikuwaje? Maswali: je kulikuwa na ukweli dhidi yake kuhusiana na tuhuma za Kamati? Ama Kamati ilitumika vibaya na mahasimu wake? Yeye amekana, sasa wanakamati inabidi wamjibu watuweke wazi, na wamjibu kwa uwazi bila kuficha, maana kama alionewa ijulikane na sisi tuliohuzunishwa ama kufurahishwa na Bunge wakati ule tuujue ukweli. Yeye anasema hakuhusika na ndiyo maana Kamati ya Mwakyembe haikuona haja ya kumwita kumhoji. Ukweli tunauhitaji sana leo kuliko jana. Ukweli huu ni haki yetu.
Kama Kamati ilimuonea, basi imuombe radhi na ituombe radhi watanzania wote. Kama kweli Mhe. Lowassa atagombea Urais Twentyfifteen, itakuwaje kwenye mijadala ya uchaguzi na CCM itasimamaje (kama itampitisha kuwa mgombea) kumuombea kura wakati ilimuangusha Bungeni kutoka kwenye nafasi nyeti ya Uwaziri Mkuu? CCM itatoa majibu gani kuhusu kwa nini ilimuita 'gamba' na ikatangaza hadharani kuanza mchakato wa kuvua magamba (ambao haukukamilika). Nilisema jana, Mhe. Lowassa amefungua pandora box, na kama atatangaza kweli kuwania Urais, inabidi haya mambo yawekwe wazi, yamalizwe, maana hauwezi jua ya kesho - ikitokea akawa mgombea wetu, tutaanzia wapi kumnadi na kusema ni mtu safi, muadilifu, anayechukia rushwa na ubadhirifu na kwamba anafaa kuwa Rais, wakati juzi tulisema hafai kuwa Waziri Mkuu na tukamtoa? Nilisema jana kuwa , CCM haipaswi ku-risk kuteua wagombea wenye mambo mengi ya kutolea maelezo kwa wananchi, ikifanya hivyo itaangushwa asubuhi ya saa nne. Watanzania wa leo siyo wa juzi.
9 comments:
AKSANTE SANA BROTHER KINGWANGALA.
Sifa umezitaja hapo mwanzo. Kama kweli watu wanasoma vizuri ulichokiandika. Hapa USA.. kiongozi bora ni yule anaye achia madaraka pale anapotajwa kwenye issue yoyote... hata kama hajausika.... kwetu naona nikinyume. LOWASA anafaa saaana. Jiulize ni kiongozi gani kutoka vyama vya upinzani ambaye ni msafi wakati wote wanapokea rushwa kutoka serikalini? RUZUKU kila mwezi. Na bado wanataka kuwa vinara wa nchi. ...sina shida ya CCM lakini ninamwamini Lowasa.
lowassa hatufai anangona kutafuta kura kwa walala hoi na watu walio wajuu.yeye ndo ametupeleka katika hali hii mpaka hii leo tunalipa umeme mara mbili mbili.afya yake ni tete,alikuwa waziri wa mazingira,hali ni tete,alikuwa waziri wa maji hali ni tete,alikuwa waziri wa ardhi viwanja vinauzwa kama njungu hali ni tete kajimegea ka ranch na kukifanya kake kule tanga,anautaka kwa uvumba na udi uraisi tumulize akiukosa atafanyaje atajinyonga na akiupata atawalipizi kisasi walio mponda?kisawa wahonga wana NEC NA friend of lowassa na tujiulize ni wakina nani.
yani ni fisadi wa kutupwa lakini sitoshanga atakapo pitishwa na kuwa raisi wetu kwa sababu watanzania hatujitambui na hatuna moyo wa uzalendo kama wenzetu nchi za jirani.
bro kingwangwala na usomi wake wote kaacha fani yake kisa tamaa ya fedha kawa mshereheshaji siku hizi kama lowassa.mmh hivi udoctor hakufai tena unataka kuwa na wewe fisadi?
UKWELI JAMAA ANA FAA SANA KAMA PESA ANAYO HATO INGIA NA TAMAA YA KUIBA KAMA HAOMNAOTAKA WAPA DRAL GIVE A GUY A BREAK MUONE WOTE MAAJABU ATAYO FANYA BIG UP LOWASA
Kwanza kabisa Kigwangalah wewe ni mbinafsi, Hilo jina si lako ina maana ulienda kurudia shule na kujichukulia jina la mwanafunzi mwingine ukawa repeater, kimsingi imeonyesha ubinafsi na ulafi hivyo huwezi kucheza "level field' hiyo imevuruga sifa yako ya uadilifu. Pili kwenye kura za maoni kugombea ubunge ulishika nafasi ya tatu,kutokana na ukaribu wako na mama Salma wa WAMA ukapitishwa wawili waliokuwa mbele yako wakakatwa- Huo ni upendeleo mkubwa, umewanyima haki waliostahili hivyo unategemea kubebwa siku zote hivyo hufai.
Tatu huna experience ya kutosha kuwa hata mbunge......sembuse rais wa nchi? Term moja ya ubunge hata haijaisha vizuri unawaza utakuwa rais? HELL NO HUNA QUALITY!
Nne, ushahidi ulio wazi unaonyesha kuwa ulikwepa kodi kule TRA ulivyoingiza vifaa vya tiba na vingine vya kawaida....Hivyo inaonyesha huna uaminifu hata huko unakokimbilia mawazo yako yote yanaonyesha unakimbilia ili ufaidike.
NAOMBA UJILINGANISHE NA LOWASSA AU Membe UONE TOFAUTI ILIVYO KUBWA. Unamsema Lowassa vibaya lakini huoni mabaya ya serikali inayoongozwa na mjomba wako Kikwete, kuanzia EPA, MEREMETA (Pinda alisema kuwa mambo ya jeshi anaogopa kuingilia- huyo ndiye tunamwita waziri mkuu), ESCROW, FEDHA WALIZOPEWA MAKAMPUNI KUPUNGUZA MADHARA YA RECESSION (Wewe ukiwa mojawapo wa aliyefaidika), DOWANS, RICHMOND(Mbona hamumuongelei Kikwete kwa sababu yeye ndiye aliyepitisha, kimsingin yeye rais na serikali yake yote walipitisha RICHMOND ila Lowassa aliamua kujiuzulu ili amnusuru Kikwete). Kuanzia mwanzo Lowassa alishasema yeye anajiuzulu kwa sababu ya kulinda heshima ya serikali, je ni nani nchi hii anayo ujasiri wa kujiuzulu kwa makosa ya watendaji wake wa chini zaidi ya Lowassa???? Mbona Mwakyembe akiwa waziri wa uchukuzi meli mbili zilizokuwa zikitoka Dar kwenda Zanzibar na kutoka Unguja kwenda Pemba zilivyozama na tukamtaka Mwakyembe ajiuzulu akakataa?? Hao si wa chini yake waliokosea kwa hiyo Mwakyembe alitakiwa ajiuzulu.....lakini alibisha na kukwepa jukumu lake na akamtetea waziri wa uchukuzi wa ZNZ asijiuzulu? Kwa taarifa yako bw. Kigwangalah, Lowassa ameonyesha mfano wa kuigwa siyo hao wengine wanaoiba kuanzia asubuhi hadi jioni......Hayo majengo ya kina Ridhiwani na familia ya rais yametokea wapi???
Anany. No 2. Unachemka. Usilinganishe USA na Tanzania wanakokula rushwa hata ofisi kuu! Rushwa, ufisadi vinazidi kutawala kwenye Serikali hii hii ambayo inaongozwa na chama chetu CCM na Lowassa ni mwanachama aliyebobea! Kama kweli anawatakia mema waTanzania mbona hajasema lolote kuhusu mgawo mkubwa wa ESCROW na mabillioni yanayotafunwa mchana kweupe na hata Rais Mwenyewe amehuzunishwa na hilo kwa mana hiyo naye anaondoka madarakani akiacha nchi imegubikwa na matatizo ya fedha!! Tuwe wakweli na kama unaishi US hujui shida za waTanzania ona shilingi iko wapi na dola inaenda wapi!! Yote hii ni frdha waliyokwapua mchana kweupe. Soma taarifa ya CAG kuna nini wanachowaambia waTanzania???? Apewe nani.???
Report ya Dr. Mwakembe kuhusu sakata la Richmond inaonyesha kuwa kulikuwa na shinikizo la Lowassa ili ile tenda apewe Rochmond. Sasa sijui unataka kutueleza nini?
Huyu no: 7 ni sawa na Nkurunzinza.... Lowasa kaondoka madarakani kulinda. kikwete kila mtu anajua hilo. Haya yote utayasikia baada ya uchaguzi. Kwa taharifa yako...hata kama Lowasa atajiunga na kambi ya upinzani bado atashinda. ... sina tatizo na vyama vya siasa lakini hawa watu hawawezi kuitetea haki ya Mtanzania. Waache kupokea hizo Rushwa (Ruzuku) kutoka ccm. Kila mtu ana makosa yake... Lowasa anawezakuwa si mkweli kwako kwasababu upo nje ya nchi,lakini waliopo vijijini hawawezi kujua makosa yake. Na hata wewe unaropoka tu, hujui ki undani alichokifanya. Mkisikia zitto kasema lile basi na nyie mnaelekea hukohuko....akisema Dr slaa ndo kabisaaaa....lakini mnashindwa kuelewa kuwa hawa watu wote wanatafuta Kazi. Na wananchi ndiyo majaji. Ndugu yangu Mtanzania... Marekani ina watu kama 400,000,000 vyama vyote nikama 5 hivi. Tanzania 40,000,000 vyama 22..... hata wewe ukienda kesho au ukitaka kuanzisha chama utapewa...kisa Ruzuku. Pesa ya bureeeee. Hii ni Rushwa na vyama vya upinzani kamwe havitakuja kushinda hata siku 99. .....acheni ushabiki wa Simba na Yanga. ...asante saana.
Post a Comment