ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 11, 2015

Halima Mdee akatisha ziara Yake Mafia

Baada ya kutoka Mafia na kufanikiwa kufanya mkutano mkubwa ambao watu zaidi ya 50 walijiunga na Chadema.

Hatimaye Mh. Halima Mdee aliamua kukatisha ziara yake Huko mafia na kurudi jimboni kwake ambapo leo alikuwa na ziara ya kutembelea jimbo zima kujionea na kuwapa pole waathirika wa mvua zilizo nyesha kwa siku 2 mfululizo.

katika ziara hiyo mbunge ameambatana na Janeth Rithe, Esther Samanya, Matha charles, Pamera Maasay na Manase Bussah.

Akizungumza na wananchi hao mdee amesema matatizo yaliyotokea na yanayo endelea kutokea ni kutokana na serikali ya CCM kushindwa kufikiria vizuri 
Hivyo amewashauri wananchi hao kuwa ifikapo mwezi wa 10 waichague Chadema/Ukawa kwani serikali iliyopo imeshindwa kutatua kero zao.

Pia amekabidhi unga na mchele pamoja na sukari vyenye thamani ya tsh.milion 5.

No comments: