Kuna wakati Beyonce na mumewe Jay Z waliamua kuishi hotelini kwa muda wakidai hawajaona nyumba ya kununua kwa ajili ya wao kuweza kuishi.
Ni hivi karibuni Jay Z ametajwa na jarida la Forbes kushika nafasi ya tatu kwa utajiri akiwa na zaidi ya dola milioni 500 kwa mastaa wa Hiphop wenye utajiri mkubwa zaidi.
Sasa stori iliyochukua headlines ni wawili hao ni kuamua kununua nyumba ya kifahari yenye thamani ya dola milioni 4 iliyopo New Orleans Garden, Marekani.Jengo hilo kabla ya kukarabatiwa lilikuwa ni makumbusho.
No comments:
Post a Comment