Advertisements

Sunday, May 17, 2015

Harambee ya Kumchangia Mohammed (Mtoto wa BI.MOZA) Kwenda kwenye matibabu India

Ndugu zetu wa Tanzania wote msaada unahitajika kukamilisha gharama za matibabu ya kumpeleka ndugu yetu India kwa ajili ya kufanyiwa Kidney Transplant kwa haraka iwezekanavyo; kwa hivi sasa mgonjwa amelazwa katika hospital ya Muhimbili, Dar-es-Salaam.

Harambee itafanyika Kama ifuatavyo:
Siku: Sunday - May 17, 2015 * SAA: Kuanzia 2pm-6pm

Address: Sligo Ave. PAB - Sligo Ave. Neighbor Park (Sligo Urban) 

500 Sligo AVE 

Silver Spring 
MD, 20910

Bank Of America Donation Account 4460 3357 9463 Moza Khamis

 Unaweza pia kutuma mchango wako hapa:
 http://www.gofundme.com/ub8rtvc

Kwa taarifa zaidi tafadhali wasiliana na:

Bi.Moza (240)467-4543
Mariam wa Talib (240)413-3341
Asha Hariz (703)624-2409
Major Mlima (301)806-8467
Shamis (202)509-1355

Ukipata taarifa hii tafadhali mjulishe mwezio.

6 comments:

Anonymous said...

Pamoja tunaweza tuungane jamani leo kwako kesho kwangu...tujumuike kwa wingi tuweze kumsaidia mwenzetu..

Anonymous said...

WATU WA DMV HATUJITAMBUI

KUUGUA, KUFA, KUKOSA AJIRA N.K. YOTE NI MITIHANI YA MAISHA AMBAYO KILA MMOJA WETU WAKATI WOWOTE ANAWEZA KUPATA MTIHANI MMOJA AU ZAIDI YA MMOJA YEYE AU FAMILIA YAKE AU RAFIKI YAKE NA WENGINEO.
LAKINI HEBU TUTIZAMENI SUALA HILI TUNALICHUKULIA KIVIPI? NAOMBA TUWE WENYE KUTAFAKARI NA KUJITAMBUA, IMEFIKA MUDA WA KUANDIKA KUWA WATU WA DMV HATUJITAMBUI! HII NI KUTOKANA NA KUFANYA MAMBO KINYUMENYUME.
KIJANA ANAUMWA NDIO HATUKATAI NA ALLAH ATAMPA UZIMA WAKE.
LAKINI KWANINI WATU WASITOE MICHANGO YAO KWA WAKATI WAO TOFAUTI NA KUMPELEKEA BI MOZA NA WAHUSIKA WENGINE AU IKAWEKWA ACCOUNT YA KUWEKA HELA? KWANINI KUWE NA HARAMBEE? HII NI KUZUSHA MAMBO AMBAYO KIMSINGI YANAWEZA YAKAPELEKEA SASA KILA ALIEKUWA NA MGONJWA WAKE NAE AKATAKA AFANYE HARAMBEE, SIONI SABABU YA KUWA NA HARAMBEE, KAMA UMEKUSUDIA KUTOA WEWE TOA TUU SIO LAZIMA KUKUSANYIKA WATU IKAWA TENA KUPIGIANA MINADA NI KUPOTEZA MUDA NA KUJITIA SHUGHULI ZISIZOKUWA ZA MAANA.
WALIOKUWA WANA UJUZI WA KUFAHAMU WATAKUWA WAMEFAHAMU VIZURI SANA NINI NINACHOSEMA.
TUSIFANYE MAMBO AMBAYO SIO YA MSINGI. ASIJE MUNGU AKAWA ANATULETEA BALAA TUU KILA SIKU KUTOKANA NA SISI WENYEWE KUOMBA KULETEA MABALAA HAYO.
TUJITAMBUE, TUJIJUE WATU TULIKOTOKA, WAPI TULIPO NA WAPI TUNAELEKEA.
ASANTENI

Anonymous said...

Unajionyesha kwamba hujawahi kufikwa na Mitihani, ndio maana umepata Muda wa Kuandika uliyo jisikia kuandika. Mungu awe Nawe na KAA Nyumbani Pumzika sio Lazima Msaada WAKO.

Ila Ukae Ukijua Iko Siku(Kwani Wewe ni BinaAdam si Malaika) Mungu atakupa Mtihani na Utahitaji Watu Wakushike Mkono, sio Lazima Kwa Harambee hata kwa Kukupa Pole au kukwambia we are here for you! Ndipo utakapo tafakari uliyoyaandika, Pindi Mwaka. Leo Kwake; Kesho Kwangu!

Anonymous said...

NDIO MAANA NIKASEMA

'WALIOKUWA WANA UJUZI WA KUFAHAMU WATAKUWA WAMEFAHAMU VIZURI SANA NINI NINACHOSEMA'.
INAVYOONYESHA UELEO WAKO BADO UPO CHINI MUNGU ATAKUSAIDIA.
NAENDELEA KUSEMA KUWA HARAMBEE SIO SULUHISHO YA MATATIZO, BI MOZA TUTAMFUATA NA TUTAMPA TULICHOKUWA NACHO ILA KWENYE HARAMBEE SITOKUJA NA WALA SISAPOTI MTU YOYOTE KWENDA KWA SABABU NI MAMBO AMBAYO YATAKUJA KUWA BAADAE BAADHI YA WENYE WAGONJWA WATATAKA IWE TENA KUVUTANA.
KWA HIVYO KUEPUSHA HAYO YASIAZWE MAMBO AMBAYO HAYANA MSINGI.
AHSANTENI.

Tumaini Geofrey Temu said...

4 DONATIONS RECENT

$60
Tumaini Temu
4 mins ago
Ugua pole
$40
Dennis Charles
9 hours ago
$50
Jabiri Jongo
14 hours ago
$50
Raymond Abraham

Anonymous said...

Nimewahi kusema siku za nyuma, lakini nitasema leo tena! Ujamaa wetu una kasoro nyingi za kiufundi. Kimsingi, tunapaswa kushirikiana katika raha na katika shida, lakini ukweli ni kwamba wana DMV na wabongo kwa ujumla tunashirikishana zaidi kwenye shida. Katika raha, wanaoshirikishwa ni ndugu na marafiki wa karibu tu, lakini katika shida wabongo tuko tayari kushirikisha wabongo popote walipo katika uso wa dunia hii. Mgonjwa yuko Bongo au msiba umetokea Bongo, wana DMV (na wabongo wote kwa ujumla) lazima washirikashwe, lakini harusi, baby shower, birthday, etc. lazima uwe ndugu au rafiki wa karibu kushirikishwa. Fairness iko wapi hapa? Afadhali tushirikishane shida zinazotupata hapa hapa DMV, lakini kwa zile zinazotokea Bongo tushirikishe ndugu na marafiki wa karibu, ambao tunawashirikisha kwenye shughuli zetu zote (raha au shida).