Kwa nini nimeanza kwa kusema maneno hayo? Ni kwa sababu nimebaini wapo ambao wamekuwa wakitumia nguvu kubwa sana kuhakikisha wanawapata wale ambao wametokea kuwapenda.Unamkuta mwanaume f’lani katokea kumzimikia msichana flani, anatumia maneno matamu, anatumia pesa na kila aina ya ushawishi kuhakikisha anampata.
Hiyo imekuwa ikifanyika sana mtaani. Wapo wanaume ambao nawajua wametumia pesa zao kuhonga hadi zimeisha lakini hawakufanikiwa kupata penzi la kweli.Wapo wafanyabiashara wengi tu ambao wametumia sehemu kubwa ya faida na wengine wakatumia mpaka mtaji kuwapa wanawake waliotokea kuwapenda lakini mwisho wa siku waliambulia patupu.
Wengine wakahonga magari na vitu vingine vya thamani lakini kuonesha kuwa penzi la kweli haliwezi kupatikana kwa kutoa kitu, waliishia kunawa tu.Achilia mbali hao wanaume, wapo wanawake ambao nao wamekuwa wakitumia njia mbalimbali kuwashawishi wanaume wawapende.
Unamkuta mwanamke na pesa zake anadiriki kumpa mvulana kila kitu ilimradi awe naye na apate ile furaha anayoihitaji.Kimsingi wengi wamekuwa wakitumia njia za kulazimisha wapendwe bila kujua kwamba, kama hawapendwi hata watoe nini hawawezi kupendwa!
Nalazimika kuyasema haya baada ya wiki iliyopita kuzungumza na mmoja wa wasomaji wangu aliyejitambulisha kwa jina moja la Nadhifa, mkazi wa Arusha ambaye alinipa kisa cha kusikitisha sana. Huyu ni msichana ambaye anatokea kwenye familia yenye uwezo kifedha lakini alichokuwa anakikosa ni penzi la kweli kutoka kwa mwanaume aliyempenda.
Kwa maelezo yake anadai alitokea kumpenda kijana mmoja, aliamini huyo ndiye mume wa maisha yake.
Alichokosea sasa ni kwamba, baada ya kujua kwamba analo penzi la dhati kwa mwanaume ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini, alianza kumpa zawadi za hapa na pale, wakati mwingine pesa.
Mwanaume naye kama walivyo wanawake wengi wa mjini kupenda mteremko, alipobaini kuwa binti huyo kamzimia, akawa anamkubalia kuwa na yeye anampenda kumbe ni usanii mtupu. Basi binti wa watu akajiaminisha kuwa amepata mwanaume, akajiachia. Alichokuwa akifanya Nadhifa ni kuhakikisha kila anachohitaji mwanaume huyo anampatia.
Itaendelea wiki ijayo.
GPL
No comments:
Post a Comment