ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 11, 2015

JK: UMECHIMBA KABURI LA VYOMBO VYA HABARI?

 Na Bryceson Mathias

WAKATI Serikali ikionesha kama inatengeneza Mazingira ya Ukiritimba wa kuvichimbia Kaburi Vyombo vya habari kwa kupitisha Sheria ya Takwimu na Makosa ya uharifu wa Kimtandao;  

Wananchi wa Kada mbalimbali nchini, na Wadau wa Habari, wanahoji, Rais Jakaya Kikwete, kusaini Miswada hiyo, anavichimbia Kaburi Vyombo vya Habari na Waandishi?.

Wana Zuoni na Waswahili wa Medani za Semi, husikika wakisema, Kwa kawaida, Ng’ombe, anaweza kutikisa Mkia wake; Lakini kwa dhati, ni agharabu, Mkia hauwezi kumtikisa Ng’ombe.

Sheria hizo ambazo zimelalamikiwa na Wadau, kwamba ni Umangimeza wa Kisiasa wa Watawala,  kuvinyanyasa na kuviziba mdomo vyombo vya habari na Waandishi; Wamesema, kama ilivyokuwa kwa Mordekai; Wanatafsiri Sheria hiyo itawafunga Mawaziri na Serikali yenyewe.

Katika nyakati za Utawala wa Mfalme Ahasuero kwenye Biblia Sura ya 7:6-10, Mordekai alikwenda kwa Mfalme kinyume cha utaratibu, ili kuwanusuru wananchi waliouzwa ili Waharibiwe, Wauawe, Waangamizwe na kuwa Watumwa na Wajakazi.

Mbinu hizo zilipangwa na Akida Mkuu wa Mfalme Ahasuero, Hamani, ambaye alitaka, Mordekai anayewatetea Wananchi Wasiharibiwe, Wasiuawe, Wasiangamizwe na kuwa Watumwa na Wajakazi; Atundikwe kwenye Mti, ukombozi wao usifanikiwe, na watu waendelee kuteseka!. Je iwe hivyo na kwa Watanzania?.


Hamani alimwambia mfalme Ahasuero, “Kuna taifa moja waliotawanyika na kukaa mahali mahali katikati ya mataifa walioko katika majimbo yote ya ufalme wako; Nao sheria zao zimefarakana na sheria za kila taifa; wala hawazishiki amri za mfalme; kwa hiyo haimpasi mfalme kuchukuliana nao.

Basi, mfalme akiona vema, na iandikwe kwamba waangamizwe; nami nitalipa talanta kumi elfu za fedha mikononi mwao watakaosimamia shughuli hiyo, waziweke katika hazina ya mfalme. Ndipo mfalme alipoivua pete yake mkononi, akampa Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi”.Esta 3:8-9.

Basi, Waandishi wa mfalme wakaitwa, siku ya 13 ya mwezi; na barua zikaandikwa, kama vile Hamani alivyoagiza vyote, kwa maakida wa mfalme, na maliwali waliokuwa juu ya kila jimbo, na wakuu wa kila taifa; kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; zikaandikwa kwa jinsi la mfalme Ahasuero, na kutiwa muhuri kwa pete yake. 

Barua zikapelekwa kwa mikono ya matarishi mpaka majimbo yote ya mfalme kuwaangamiza Wayahudi wote, na kuwaua, na kuwafisha, vijana kwa wazee, watoto wachanga na wanawake pia, siku moja, yaani, siku ya 13 ya mwezi wa 12 ndio mwezi wa Adari; na kuyachukua mali yao kuwa nyara

Nakili ya andiko, ya kupigwa mbiu katika kila jimbo, ilitangazwa kwa mataifa yote wawe tayari siku ile ile. Matarishi wakaondoka wakaenda haraka kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Shushani ngomeni. 

Mfalme na Hamani wakaketi ili kunywa divai na kujifurahisha (kama vile Waziri wa MawasilianoSayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawa akifurahi kusainiwa kwa Miswada hiyo); bali mji wa Shushani ukafadhaika. 

Wadau wa Habari wanadai, yawezekana hivyo ndivyo Bunge lilivyopelekewa Miswada ya Sheria ya Takwimu na Makosa ya uharifu wa Kimtandao kwa kutumia Hati ya Dharula, isainiwe na Rais, ili kuwakomoa Waandishi na Vyombo vya habari, ikilengwa Uchaguzi Oktoba 2015, ili kuwatisha Waandishi, Wananchi wasipate nafasi ya kutoa na kupokea habari.

Kama ulivyotokea uovu wa Hamani kwa Wayahudi, Mordeikai alipojua mambo yote yaliyofanyika, alizirarua nguo zake, akajivika gunia pamoja na majivu, akatoka hata kufika katikati ya mji, akalia kwa sauti kuu ya uchungu.

Mordekai pia alifika hata mbele ya mlango wa mfalme; maana hakuna awezaye kuingia ndani ya mlango wa mfalme hali amevaa magunia. Na katika kila jimbo, ambako amri ya mfalme na mbiu yake iliwasili, palikuwako msiba mkuu kwa Wayahudi, na kufunga, na kulia, na kuomboleza; hata na wengi wakalala juu ya gunia na majivu, kama ilivyo kwa Wandishi, Wananchi na Wadau wake.

Basi tunaamni, Wananchi wasio na Sauti (Voiceless), ambao vyombo vya habari ni Mhimili wao wa Nne wa kutetea Kodi na Rasilimali zao, ambao wamewaibulia Maovu na Machafu Mengi, (Richmond, Dowans, EPA,  wa Wanyama Pori, na hivi karibuni Escrow), watapiga Kelele.

Wanahabari tunaamini, Kelele zinasikilizwa, na tuna mifano ya kelele kusikilizwa, ‘Migomo ya Wafanya Biashara, Migomo ya Madereva, Wanavyuo, Walimu, Madaktari na Wauguzi, Wakulima, Wananchi wanaodai Ardhi, Matokeo ya Uchaguzi ya kughushi, yameiipa Serikali wakati Mgumu.

Mordekai aliagiza wampelekee Esta jibu la kusema, “Wewe usijidhanie kuwa utaokoka nyumbani mwa mfalme, zaidi ya Wayahudi wote. Kwa maana wewe ukinyamaza kabisa wakati huu, ndipo kutakapowatokea Wayahudi msaada na wokovu kwa njia nyingine; hivyo wanadishi na wadau, msidhani mtaokoka.

“Ila wewe utaangamia pamoja na mlango wote wa baba yako; walakini ni nani ajuaye kama wewe hukuujia ufalme kwa ajili ya wakati kama huo?tusaidiane kupiga kelele ya kupinga uovu huu!.

Esta aliingia kwa Mfalme bila Utaratibu, akakubalika, na akahakikisha badala ya Mordekai kutundikwa kwenye Mti aliouandaa Hamani, akatundikwa yeye. Waandishi tushikamane kukataa unyannyaswaji huu wa kutuziba mdomo!

katika Esta 7:8-10 inasema,  Kisha mfalme akarudi kutoka katika bustani ya ngome hata mahali pa karamu ya divai. Ikawa Hamani amejitupa chini penye kitanda alipokuwapo Esta. Mfalme akasema,
‘Namna gani! Je! Atamfanyia malkia jeuri hata machoni pangu nyumbani mwangu? Na neno lilipotoka kinywani mwa mfalme, wakamfunika uso Hamani’. 

Ndipo aliposema Harbona, msimamizi-wa-nyumba mmojawapo wa wale waliohudhuria mbele ya mfalme, Tazama, basi, mti wa mikono hamsini urefu wake, Hamani aliomwekea tayari Mordekai, ambaye alinena vema kwa ajili ya mfalme, upo umesimamishwa nyumbani kwa Hamani. Mfalme akasema, 

Mtundikeni juu yake. Basi wakamtundika Hamani juu ya mti aliomwekea tayari Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia; Hivyo pamoja na kwamba Sheria hizo zimelenga kuwakomoa Waandishi na Vyombo vya habari; Sheria ya Takwimu  kisiasa, zitawafunga Mawaziri.

Kwa nini nasema na kurudia hayo; kwa sababu watatoa bungeni taarifa za wizara zisizo sahihi, na itakapofuatiliwa, wataonekana wamesema Uongo.

No comments: