ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 5, 2015

KAMISHNA WA FORODHA NA ULINZI WA MIPAKA WA MAREKANI ATEMBELEA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Waziri wa  Mambo ya Ndani   ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (kushoto), akizungumza na Kamishna wa Forodha na Ulinzi wa Mipaka toka Serikali ya Marekani Bw. R. Gil Kerlikowske alipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia masuala ya ushirikiano wa shughuli za kiulinzi kati ya Serikali ya Tanzania na Marekani. Kulia ni Msaidizi wa Balozi wa Marekani hapa nchini Bi. Virginia Blaser.
Kamishna wa Forodha na Ulinzi wa Mipaka toka Serikali ya Marekani Bw. R. Gil Kerlikowske (kulia), akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo  ya  Ndani  ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe wakati wa mazungumzo yaliyofanyika Ofisini kwa Waziri Chikawe kuhusu kuimarisha ushirikiano wa masuala ya kiulinzi kati ya Serikali ya Tanzania na Marekani.
Ujumbe kutoka Serikali ya Marekani wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani  ya Nchi Mhe. Mathias Chikawe alipokuwa akizungumza nao wakati walipotembelea Ofisini kwa Waziri Chikawe.  Ujumbe huo uliongozana na Kamishna wa Forodha na Ulinzi wa Mipaka toka Serikali ya Marekani Bw. R. Gil Kerlikowske.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mathias Chikawe (kulia), akizungumza  na Kamishna wa Forodha na Ulinzi wa Mipaka toka Serikali ya Marekani Bw. R.Gil Kerlikowske (katikati) wakati akiondoka mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ofisini kwa Waziri Chikawe.  Kushoto ni Msaidizi wa Balozi wa Marekani hapa nchini Bi. Virginia Blaser.

No comments: