ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 5, 2015

KUNDI LINGINE LA WATANZANIA 40 WALIOKUWA WAKIISHI NCHINI YEMEN WAREJESHWA NYUMBANI LEO


Awamu ya tatu ya Kundi la Watanzania waliokuwa wakiishi nchini Yemen, wameendelea kurudishwa nyumbani kutokana na mapigano yanayoendele nchini humo. Watanzania 40 ambao walikimbilia nchini Oman kutokea Yemen, wamefanikiwa kusafirishwa leo chini ya usimamizi wa Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mh. Ali Ahmed Saleh.
Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mh. Ali Ahmed Saleh akizungumza na Baadhi ya watanzania waliokuwa wakiishi nchini Yemen, ambao wako safarini hivi sasa kurudishwa nyumbani baada ya mapigano yanaoendelea nchini humo.

No comments: