Mama alitabasamu wakati unalia mama alijifanya uchizi ili kukufurahisha ghafla ungetokea kuwaona mtoto anapocheza na mama yake ungelidhani wote ni watoto kwa mapenzi ya mama.
Mwanadamu tambua unaweza umizwa na wengi lakini upendo wa mama ukakufanya utulie na hakuna mapenzi ya kweli kwa mtu kama mapenzi ya mama.
Mama juu yako baya likikukuta mama hulia mama yupo tayari kudanganya ulimwengu kukukomboa katika matatizo yako.
Alificha chakula wakati ukicheza udogoni na uliporejea ukamkuta amelala lakini aliacha maagizo utakuta wapo wa kukupashia yote mapenzi.
Mama alipoamka mwanzo alikuulizia ameshakula? Ima umekula atafurahi ima hujala atapita majumba ya watu kukuulizia hata kama atatoka miguu peku yote mapenzi tu.
Ulipoumwa usiku halali atataabika kwa kukaa na wewe ukiwa mikononi mwake huku akilalila ukuta pembeni mwa kitanda huku akitarajia pakikucha shingo limuume kwa kukesha na wewe yote mapenzi hayo.
Mtu yoyote akikupenda watu watamshangaa kwanini anakupenda sana? Lakini mapenzi ya mama hayaulizwi kwanini anampenda yote ni nguvu za hisia za upendo toka kwa mama.
Umekuwa sasa huenda hayupo tena mama amekuacha katika dunia ya mihangaiko na wala tambua hakuna tena kiumbe kitachokupenda kama alivokuwa mama.
Na ukiwa umebarikiwa upendo ulio hai kwako namaanisha uhai wa mama basi huenda amechokaa na anatembea kama mtoto sasa rudisha upendo wako kwa kumfanya nae afurahi japo hutoweza kulipiza yote.
Mama utamkumbuka utapomkosa utatamani kuita mama na hata ukipata wa kuwaita upendo hautatoka moyoni.
Wakati ulipotoka alitabasamu basi na wewe hakikisha wakati anakukimbia duniani mfanye atabasamu hata kama atatokwa na machozi .
Mtumie ujumbe huu Mama na kama hunae tena muombe kwa MOLA upatapo ujumbe huu watumie wenzako huenda wakafufua hisia kwa Mama.
HUYU NDIO MAMA WA UPENDO.
KISIWA CHA IMANI
HAPPY MOTHER'S DAY KWA MAMA WOTE DUNIANI
No comments:
Post a Comment