Advertisements

Friday, May 22, 2015

Minziro awadaka wote waliotemwa Yanga


Kocha Mkuu wa JKT Ruvu, Felix Minziro.

Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam
SIKU chache baada ya Yanga kudaiwa kuwa ina mpango wa kuwatema nyota wake 11 wa kikosi hicho, Kocha Mkuu wa JKT Ruvu, Felix Minziro, ameibuka na kuomba apatiwe wachezaji hao.

Baadhi ya wachezaji ambao Yanga inadaiwa kutaka kuwafungashia virago klabuni hapo ni Jerry Tegete, Hussein Javu, Danny Mrwanda, Nizar Khalfan, Rajabu Zahir, Edward Charles na Hassan Dilunga sababu ikiwa ni kushindwa kuonyesha uwezo wa juu.

Minziro, kocha na mchezaji wa zamani wa Yanga, ameliambia Championi Ijumaa kuwa, endapo Yanga itawaondoa wachezaji hao, anaamini watamsaidia katika harakati zake za kuhakikisha JKT Ruvu inakuwa vizuri msimu ujao.“Nimesikia kuwa Yanga wanataka kuwafungashia virago wachezaji hao kwa madai kuwa wameshuka viwango, kama vipi wanipatie mimi, siyo mmoja au wawili, nawataka wote,” alisema Minziro.
CREDIT:GPL

No comments: