Advertisements

Saturday, May 30, 2015

MWENGE WA UHURU WAKIMBIZWA WILAYA YA KINONDONI MKUU WA WILAYA ATANGAZA AJIRA YA PAPO KWA PAPO

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiwa ameubeba mwenge wa Uhuru baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto), akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda baada ya kumaliza mbio zake wilayani humo Dar es Salaam jana asubuhi. Mwenge huo ulianza mbio zake Wilaya ya Ilala na kuzindua miradi mbalimbali.
 Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum (kulia), akisalimia na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda.
 Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Kinondoni wakiwa wamejipanga katika foleni wakisubiri kuupokea mwenge wa Uhuru kabla ya kuanza mbio zake wilayani humo.
 Wakimbiza mwenge kitaifa.
 Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa (kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
  Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum akivuta pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ya mradi wa maji Mburahati Barafu na Kisiwani uliofadhiliwa na Jumuia ya Ulaya, Serikali ya Ubelgiji na Serikali ya Tanzania  wakati wa ukimbizaji wa mwenge huo Wilaya ya Kinondoni humo.
  Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum akivuta pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ya baabara tatu katika Shule ya Sekondari ya Makulumla. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Beatrice Mhina.
 Mwanafunzi Noel Mwita wa Shule ya Sekondari ya Makulumla, akiekeza namna ya kuchanganya madawa wakati kiongozi huyo wa mwenge, Juma Chum (wa nne kushoto), alipoweka jiwe la msingi za maabara katika shule hiyo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Beatrice Mhina, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda
 Vijana wa hamasa wa wilaya ya Kinondoni wakitoa burudani mbalimbali wakati wa kuupokea mwenge huo ukitokea wilaya ya Ilala.
  Vijana wa hamasa wa wilaya ya Kinondoni wakitoa burudani mbalimbali wakati wa kuupokea mwenge huo ukitokea wilaya ya Ilala.


 Wananchi wa Mburahati wakiupokea mwenge huo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji katika eneo hilo.
 Vijana wa hamasa wakipamba hafla hiyo kwa kuonesha matukio mbalimbali.
 Mwanamuziki Rehema Chalamila 'Ray C' akitoa ushuhuda wa jinsi alivyoacha matumizi ya dawa ya kulevya mbele ya Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa kituo cha vijana walioathiriwa na dawa hizo katika Hospitali ya Mwananyamala.
 Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka 2015, Juma Khatibu Chum, akimkabidhi Amina Mshana chandarua kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa malaria.
Wakimbiza mwenge wa Uhuru kitaifa,  Delina Simfukwe (kushoto) na Bakia Abdallah wakiteta jambo na mwanamuziki RehemaChalamila 'Ray C baada ya kutoa ushuhuda kuhusu matumizi ya dawa za kulevya.


Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ametoa ajira ya moja kwa moja kwa kijana Yusuf Mzitto mtaalamu wa masuala ya kompyuta ambaye alikuwa ameathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya  wa wilaya hiyo.

Makonda alitoa ajira kwa kijana huyo mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka huu. Juma Khatibu Mchum wakati wa uzinduzi wa kituo cha vijana walioathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya kilichozinduliwa na kiongozi huyo wa mbio za mwenge katika Hospitali ya Mwananyamala Dar es Salaam jana asubuhi.

"Kijana huyu mwenye elimu ya juu ya masuala ya kompyuta alikuwa ameathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya hivyo baada ya kuacha kutumia dawa hizo tumempa ajira katika ofisi yangu ili aweze kufanyakazi badala ya ujuzi wake kupotea bure" alisema Makonda.

Makonda alisema kuwa katika kuwawezesha vijana walioathiriwa na dawa hizo wamepatana na viongozi wa manispaa hiyo kuwa kila kampuni inayofanya shughuli za kijamii katika wilaya hiyo ili iweze kupata tenda ya kufanya kazi yoyote ni lazima itoe mchanganuo  kwanza wa utoaji wa nafasi ya ajira kwa vijana wa wilaya hiyo.

Alisema wamechukua hatua hiyo ili kutoa fursa ya ajira kwa vijana waliohamua kuachana na matumzi ya dawa za kulevya ambao hawana kazi hivyo kupitia  kakampuni hizo ziweze kuwasaidia vijana hao baada ya kupatiwa tenda na manispaa hiyo.

Alisema ili kuunga jitihada za Rais Jakaya Kikwete za kupambana na uingizaji wa dawa za kulevya ameanzisha mpango wa kukutana mara moja kila mwezi na vijana walioathiriwa na dawa hizo ili kubadilishana mawazo badala ya kuwatenga.

Makonda alisema vijana hao wengi wao ni wataalamu wa masula mbalimbali akimtolea mfano kijana aliyepewa ajira katika ofisi yake ambaye atawasaidia katika mambo mengine.

Akizungumzia mbio za mwenge katika wilaya yake kwa mwaka huu alisema umezindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi saba yenye jumla ya sh.5,079,153,972 ambapo kati ya fedha hizo sh.14,802,200 ni fedha kutoka serikali kuu, sh.2,672,992 kutoka katika Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni, sh.913,800,780 ni mchango wa wahisani na sh.1,477,978,000 ni michango ya wananchi.

Alitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa maji, ujenzi wa barabara, ujenzi wa baabara, ujenzi wa shule za Sekondari, ujenzi wa jengo la wazazi, ujenzi wa ofisi ya Kata na ujenzi wa nyumba ya walimu.

Alisema mwenge huo ulipata fursa ya kukagua miradi endelevu wa ugawaji wa vyandarua, mradi wa wanawake wajasiriamali, mradi wa vijana wajasiriamali watunzaji wa mazingira na mradi wa huduma za ukimwi.

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Juma Khatibu Chum aliwataka watanzania wote bila ya kujali itikadi za vyama vyao kudumisha amani na utulivu wa nchi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.

Alisema amani ya nchi tusipo kuwa makini inaweza kuharibiwa kwa siku moja wakati imetafutwa kwa miaka mingi na aliwata vijana kuacha kutumia dawa za kulevya na kujikinga ma malaria ambayo yame kuwa yakiua watu wengi kuliko ukimwi. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

No comments: