Advertisements

Monday, May 25, 2015

VIJANA WAWEKWA DARASANI NA WAZEE DMV WACHAPWA 5-3

 Timu ya Wazee
 Timu ya Vijana

Timu ya wazee DMV imedhihirisha kwa mara nyingine kwamba Vijana bado ni chamtoto katika kusakata kabumbu baada ya kukubali kipigo cha goli 5-3 katika mechi iliyochezwa viwanja vya Meadowbrook park, Chavy Chase Maryland mechi iliyoambatana na nyama choma.

Timu hiyo ya Vijana ikiongozwa na kocha wake Rich iligomea kupiga picha kabla mchezo haunjaanza kitu kilichotafsiria na wengi ni kuona dalili za kupoteza mchezo huo mapema.

Katika mechi hiyo timu ya Wazee iliendelea kuonyesha ubabe katika mechi hizo zinazochezwa mara kwa mara hapo DMV.baada ya kushinda mechi hiyo na kufanya timu ya Vijana kupoteza mechi ya 15 mfululizo  tangia mechi hizo zianzishwe DMV miaka 17 iliyopita.

Mechi ilikua kali na ya upinzani mkubwa kwa timu ya Vijana kucheza mchezo wa pasi fupi huko mchezo ukionekana kama timu ya Vijana ingeweza kuibuka na ushindi mnono lakini kadri muda ulivyozidi kusogea timu ya Vijana ilikua ikiishiwa kasi iliyoanza nayo huku timu ya Wazee ikionokana kama ingini ya dizel kwa kuanza mpira taratibu huku wakitumia uzoefu wa kucha za mpira siku nyingi bila ya kua na papara.
 na kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo timu ya wazeew waliendelea kuwadhibiti Vijana mpaka kipenga cha mwisho Wazee 5 Vijana 3.

2 comments:

Anonymous said...

Hili tangazo mbona limekaa kiuchoyouchoyo? Wote tunakaribishwa au ni wachezaji tu? saa ngapi?

Anonymous said...

Kaka Lucas mbona unatizingua? Hizo picha mbona wengine hatukuwepo uwanjani? na tuko kwenye picha? Weka picha za ukweli kaka.