Advertisements

Sunday, May 10, 2015

RAIS JAKAYA KIKWETE TAYARI AMESHASAINI SHERIA YA MAKOSA YA MITANDAO


Rais Jakaya Kikwete tayari ameshasaini sheria yenye utata ya makosa ya mtandao na muda wowote kuanzia sasa itaanza kutumika rasmi.

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, amesema hayo leo wakati akizungumzia masuala mbali mbali yanayohusu sheria hiyo ambayo kupitishwa kwake kumesababisha malalamiko mengi kutoka kwa wadau kuwa itaminya uhuru wa habari, kuingilia faragha pamoja na uhuru wa watu kuwasiliana.
Ufuatao hapa chini ni uchambuzi kidogo kuhusu baadhi ya vipengele vilivyozua utata katika muswada huu uliokuwa umetolewa.

1. Kifungu 7 (2b): Mpokeaji wa ujumbe (receiver) anaweza kushtakiwa kwa kosa la kupokea ujumbe ambao sheria imeufanya kuwa wa jinai. (Mfano: Mtu akikuforwadia ujumbe, ukiupokea na wewe umefanya kosa la jinai).

2. Kifungu 8: Itakuwa ni kosa la jinai kama mtu ataweka wazi nyaraka za siri za serikali hata kama ni nyaraka ya kusaidia nchi kwa ujumla (Mfano: Matumizi mabaya ya mali ya umma).

3. Kifungu 14: Picha yoyote yenye mwelekeo unaoweza kuonekana kama ‘mchafu kingono’ inaweza kupelekea mtu kufungwa hadi miaka 10 au kulipa milioni 30; (Mfano: mtu kaposti picha yake ambayo sio ya ponografia lakini ‘ikatafsiriwa’ hivyo. Sheria haijatafsiri ponografia!)

4. Kifungu 23: Je, ulijua kuwa ‘kusababisha maudhi ya hisia’ kwa mtu mwingine ni unyanyasaji na unaweza kufungwa kifungo kisichopungua mwaka mmoja?

5 Kifungu 22: Ukiweka ujumbe katika mtandao na ukaufuta au kuuboresha, kama ukishtakiwa kwa kuweka ujumbe huo unaweza kuhukumiwa pia kwa adhabu ya kuuboresha au kuufuta. (Mfano: unapofuta ‘status’ zako za WhatsApp, unaweza shitakiwa kwa kuchelewesha ushahidi kisa tu ulifuta na hamna mtu anayeweza kujua ulifuta kwa kusudi au la.)

6. Mkuu wa kituo cha Polisi chochote kile nchini anaweza kuagiza wewe umpatie simu/laptop yako au taarifa zako zote (kwenye email, chats) au hata vifaa vyako au ofisi yako kwa ajili ya upelelezi bila oda ya Mahakama.

7. Serikali kupitia waziri husika ndio ina mamlaka ya kusema jambo lililowekwa kwenye mtandao ni la kweli, uongo au la kupotosha.
SOURCE:HARAKATI ZA BONGO BLOG

4 comments:

Anonymous said...

Yaani sisi weusi.,basi tu.kuanzia Leo nitajiita mzungu ili labda nitaweza kufikiri tofauti

Anonymous said...

kazi kweli hii inafaa sana ila sasa uiangalia upande mwingine wasichana wadogo wanaolewa au kufanyiwa vitendo kwa nguvu na sharia haifuatilii haya, kuna mengi sana ya kuongeza kwenye hii sharia ya mawasiliana na utendaji kwa ujumla. Watu wanapigana au kutukanana matusi mazito wazi na hata mbele ya watoto mitaani usiombe ni aibu. Unywwaji wa pombe hadharani na kuwatuma watoto pombe kwenye maduka na mabaa, kuwatuma sigara watoto pia ni mambo ya kuwekwa wazi watu wazima waache kuwapeleka watoto kwenye shughuli za sherehe hadi saa saba usiku kama huna mwangalizi basi usiende. Tuacheni kuyumba kuna mambo lukuki ya kufanyia kazi serikali iliyoko haijaweza bado tunahitaji kubadilika..

Anonymous said...

Kifungu cha 7 na 8 that's bullshit,ukishakuwa kiongozi lazima ukubaliane na challenges,nchi yetu haina FREEDOM OF SPEECH at all,SO SAD

Anonymous said...

Watu wanatukanana. Kwenye Instagram Internet yaani watanzania wamezidi .