ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, May 10, 2015

MADAI, DENTI MIAKA 12 AWEKWA KINYUMBA NA TICHA




Mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Mary Joseph.


Magida anayedaiwa kuwekwa kinyumba na ticha.

Mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Mary Joseph akizungumza na paparazi wetu alisema, akiamini mwanaye ana umri mdogo na anahudhuria masomo kama kawaida, alishangazwa Machi mwaka huu mtoto wake alipokwenda shule na kutorejea nyumbani hadi siku iliyofuata.

Aliporudi, alidai alisumbuliwa na tumbo na kwamba alipata hifadhi kwa mtu aliyekataa kumtaja.
“Siku iliyofuata usiku saa saba akaniomba funguo aende kujisaidia, alipotoka alikaa muda mrefu bila kurudi, nikamfuata na kumtafuta sikumuona.


Kesho yake nikatoa taarifa polisi kwa kuwa moyo wangu ulijawa hofu nikihisi katekwa usiku ule, siku mbili baadaye limuona kituo cha mabasi Ubungo lakini alinikimbia,”alisema mama huyo na kuongeza:

“Siku iliyofuata nilienda na kuomba msaada wa watu wakamkamata, baada ya kumpeleka Polisi Mawasiliano, akiwa analia alidai kwa kipindi cha mwaka mmoja alikuwa kwenye uhusiano na mwalimu huyo ambaye alimwambia afanye siri na alimkataza kwenda shule, akawa anamsubiri chini ya mti mmoja ambapo alimpitia kila alipotoka kufundisha na kumpeleka gesti tofautitofauti na wakiwa huko, humpatia maswali kisha kumsahihishia, kitu kilichokuwa kigumu mimi kugundua kama alikuwa haendi shule,” alisema mama huyo.

Kamanda Camillius Wambura.

Kaongeza kuwa, cha ajabu siku hiyo waliporudi nyumba alitoroka tena na mpaka gazeti hili linakwenda mtamboni hakuwa akijulikana aliko.Jitihada za kumpata mwalimu Kimweri ziligonga mwamba kwa kuwa aliacha kufundisha tokea mwaka jana na kuhamia shule nyingine iliyopo Kisarawe ambako pia hakupatikana kwa maelezo kuwa hajaonekana kwa muda mrefu. Jalada la kesi yake limeandikwa SGR/RB/1216/2015 KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI.
Credit:GPL

2 comments:

Anonymous said...

Wazazi tuna majukumu kwa asilimia mia moja kujua motto amefanya nini shuleni kila siku iendayo kwa Mungu na pia kuwasiliana na waalimu kujua kama motto amehudhuria shuleni. Inafikia wakati sasa wizara ya Elimu kuunda mtandao utakaowezesha wazazi, Waalimu na mwanafunzi mwenyewe kutuma taarifa za haraka au siku hiyo hiyo kwenye simu za wazazi endapo kuna tatizo au motto hakuonekana shuleni. Tusinganganie sharia ya mitandaoni tukasahau mambo muhimu ya kuendeleza elimu Tanznaia, siku hizi simu zipo ni kiasi cha kuunda mtandao (network) na wazazi wote watoe nambari zao ziwekwe kwenye system. Tuacheni ubabaishaji fedha nyingi sana zinapotea na kutshindwa kuweka mambo yenye msingi Tanzania hii. CCM Pumzikeni..

Anonymous said...

Serikali isifanye mchezo na Jamii ya Tanzania!
HUU UJINGA LAZIMA UKOMESHWE!
Government of Tanzania and Law makers MUST make a Law that it is illegal for all;
Educators /Professors/Teachers/ and or Staff of Any Educational Institution in Tanzania to have an affair or relationship with students or minors!
There must be penalty for such reckless behavior, such;
as If proven in the court of law, such person shall be dismissed from the employment with no benefits!
Such person will face a fine of up to $15,000 and up to 5 years in prison!

People will follow the Law!!