Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete maeno yaliyoathiriwa vibaya na mafuriko huko Tegeta wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maagizo kwa uongozi wa wilaya ya Kinondoni kuyaondoa kwa haraka maji yaliyozunguka makazi ya watu eneo la Tegeta wilayani Kinondoni kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda pamoja na Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda akiwaagiza kutafuta mbinu za kuyaondoa kwa haraka maji yaliyozingira makazi ya watu eneo la Tegeta
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia makazi holela yaliyojengwa katika bonde la mkwajuni eneo la mto Msimbazi na kisha kuongea na wakazi wa eneo hilo akiwashauri kuhama kwakuwa eneo hilo si salama kwa maisha na mali zao(picha na Freddy Maro)
1 comment:
Every year we see this ....wanatembelea na kuangalia....no solution...basi lets wait next yr tena...pole kwa walio pata matatizo....
We have a lot of engineers but tuna subiri mzungu atusaidie....tutafika
Post a Comment