Tuesday, May 5, 2015

SHULE ZA MOSHI MJINI MJADALA WA KUKUZA NA KUDUMISHA KISWAHILI NA KUINUA KIWANGO CHA ELIMU, MGENI RASMI KIJANA DAUDI MRINDOKO

Mjadala kubwa wa kukuza na kudumisha lugha ya Kiswahili ulitawala katika Debate iliyofanyika mjini Moshi,mdahalo huo uliudhuriwa na walimu pamoja na wanafunzi kutoka shule za Secondary...Korongoni Secondary / Regnal Mengi Secondary / Bendel secondary / Mother Theresa Secondary na zinginezo katika mdahalo huo mgeni rasmi alikuwa Kijana Daudi Babu Mrindoko mwenyekiti wa tahasisi ya Wazalendo Tanzania pia mjumbe wa Uvccm mkoa kilimanjaro.Wanafunzi wa shule hizo wamedhamiria kukikuza,kukidumisha na kukitumia Kiswahili kwani lugha ya kujivunia pia Kiswahili kinatambulika katika lugha kumi bora za kimataifa. Mwishoni mwa mdahalo huo mgeni rasmi bwana Daudi Mrindoko alitoa nasaha zake kwa wanafunzi hao kuwa kiswahili ni lugha ya kujivunia na niwajibu wa wanafunzi na wananchi wote kuhakikisha kuwa kinadumishwa, Bw.Daudi Mrindoko alisema kiswahili ni zawadi tuliyopewa na mungu na lazima tuidumishe na kujivunia aliongeza kusema kuna nchi nyingi duniani hawana lugha ya Taifa,pia aliwataka wanafunzi kuzidisha juhudi katika masomo yao kwa faida yao na taifa kwa ujumla.


No comments: