Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi Zuhura Hanif (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa chaneli mpya ambazo ni IROKO PLAY, IROKO PLUS, AMC SERIES na STARTIMES ZONE. Kushoto akifuatilia kwa makini uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam ni msanii wa Bongo Flava na balozi mpya wa kampuni hiyo, Nurdin Bilal au maarufu kama Shetta.
Msanii wa Bongo Flava na balozi mpya wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Nurdin Bilal au maarufu kama Shetta akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa chaneli mpya ambazo ni IROKO PLAY, IROKO PLUS, AMC SERIES na STARTIMES ZONE jijini Dar es Salaam leo.
Katika kuboresha huduma zake kampuni ya StarTimes Tanzania imezindua chaneli nne tofauti kwa mpigo za kusisimua na zilizokuwa zikisiburiwa kwa hamu kubwa na wateja wake.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amesema kuwa chaneli hizi mpya zimekuja wakati muafaka ambapo wateja wetu wengi walikuwa wakiziulizia.
“Kwa muda mrefu tumekuwa tukipokea maoni kutoka kwa wateja wetu kuhusu chaneli gani za kuongeza ili kuwafanya wafurahi na kuendelea kubaki nasi. chaneli hizi nne ni jibu tosha kwao kwani ninaimani zitakata kiu yao ya muda mrefu. IROKO PLAY na IROKO PLUS ni chaneli zilizosheheni filamu nzuri na bora zilizojishindia tuzo mbalimbali nchini Naijeria na barani Afrika kwa ujumla.” Alisema Bi. Hanif
“AMC SERIES nayo imetofautiana kidogo na hizi, yenyewe inaonyesha mfululizo wa filamu – ama‘Series’ kama wengi alivyozoea, tamthiliya, vichekesho pamoja na maigizo bora kabisa kutoka nchi tofauti za Afrika. Huku STARTIMES ZONE yenyewe ni mjumuisho wa vipindi mbalimbali vikiwemo filamu, tamthiliya, michezo na burudani, vipindi vya watoto pamoja na makala mbalimbali za uchambuzi ili kumfanya mtazamaji aburudike.” Aliongezea
“Nina uhakika kuna watu wengi ambao si wapenzi tu wa filamu zetu za nyumbani bali pia kutoka nchi nyingine barani Afrika, hususani Naijeria. StarTimes haikutaka kuwatupa wapenzi wa filamu hizo na ndio maana imefanya jitihada kubwa kwa kuingia makubaliano ili kuhakikisha inapata haki ya kuzipata na kuzionyesha chaneli hizi.” Aliendelea
“Hivyo basi napenda kuwaomba wateja wetu muanze kutazama chaneli hizi, ninaimani mtazifurahia na kuzipenda. IROKO PLAY na AMC SERIES zinapatikana katika kifurushi cha Uhuru IROKO PLUS inapatikana katika kifurushi cha Kili kwa king’amuzi cha antenna, kwa dishi itawekwa baadae kidogo. Huku STARTIMES ZONE inapatikana katika kifurushi cha NYOTA kwa ving’amuzi vyote. Ningependa kumalizia kwa kusema bado tuna mambo mengi mazuri yanakuja kwa ajili ya wateja wetu, endeleeni kutumia huduma za StarTimes.” Alihitimisha Bi. Hanif
Naye msanii wa miondoko ya kizazi kipya Bw. Nurdin Bilal au maarufu kwa jina la ‘Shetta’ kama anavyojulikana na mashabiki na watanzania kwa ujumla, ambaye kwa sasa ni balozi wa StarTimes Tanzania amesema kuwa amefurahi kuwa sehemu ya uzinduzi huo kwani una faida kubwa kwa wateja wote wa kampuni hiyo.
“Maboresho katika huduma na bidhaa ni kitu cha msingi sana katika kazi yoyote ile kwani ndicho kinachokufanya uwe mshindani na kuendelea kuwavutia wateja wengi. Huduma za matangazo ya luninga kwa dijitali ni sekta mpya na yenye ushindani mkubwa. Nafurahi kuona StarTimes wapo makini kuhusu hilo na wamejizatiti kutoa ushindani mkali kwa kuwapatia wateja wao kile wanachostahili.” Alisema msanii Shetta
“Chaneli hizi nne tulizozizindua siku ya leo ninaamini zitakonga nyoyo za wapenzi wengi wa filamu kwani ninaamini kila mtu anakipindi anachokipenda akiwa mbele ya luninga yake. Mimi mwenyewe huwa ninatazama filamu hizi kwani licha ya kuburudika pia najifunza na kujionea tamaduni za mataifa mengine ya kiafrika,” alisema Shetta na kumalizia, “Hivyo basi ningependa kutoa wito kwa wateja wote wa StarTimes mimi kama balozi wao, hivi sasa kila kitu kinapatikana kwenye king’amuzi chako, tazama chaneli hizo uburudike.”
Chaneli ambazo zimezinduliwa ni IROKO PLAY – inayoonyesha filamu kali na za kuvutia za kinaijeria na Afirka kwa ujumla za kuanzia mwaka 2007-2011, IROKO PLUS – inayoonyesha filamu kali na za kuvutia za kinaijeria na Afirka kwa ujumla za kuanzia mwaka 20012-2015, AMC SERIES – inayoonyesha mfululizo wa tamthiliya, vichekesho na maigizo bora yaliyojishindia tuzo mbalimblai barani Afrika, huku STARTIMES ZONE (ST ZONE) yenyewe imeletwa mahususi ikiwa ni mjumuisho wa filamu, tamthiliya, michezo na burudani, vipindi vya watoto pamoja na makala mbalimbali za uchambuzi ili kumfanya mtazamaji aburudike.
No comments:
Post a Comment