Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.Seif S.Rashid (Mb) Ametoa hotuba katika mkutano wa Shirika la Afya Duniani(WHO), unaoendelea mjini Geneva,Uswisi.
Katika hotuba yake ameeleza masuala mbalimbali yaliyotekelezwa na yanayoendelea kutekelezwa hususani kufikiwa kwa lengo la milenia la kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano kiwango cha watoto 54 kati ya vizazi hai 1000.
vile vile utekelezaji wa mpango wa Afya ya msingi wa 2007-2017, lengo ni kuimarisha na kuhakikisha huduma za afya zinamfikia kila mwananchi, ambapo kumekuwa na ongezeko la vituo vya kutolea huduma, zahanati katika kila kijiji na vituo vya Afya kwa katika kila kata.
Pia,alieleza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya kielektroniki ambayo itasaidia sana katika kuboresha utoaji wa huduma za Afya katika vituo vyote vya Afya.
Pia, alieza nchi ilivyopitia katika misukosuko ya kukabiliana na mbalimbali Kama Rift Valley fever,H1N1 na ugonjwa wa Dengue.vile vile, Nchi yetu haikuwa nyuma katika kukabiliana na Janga la Ebola lililotokea Afrika Magharibi ambapo tulishiriki kwa kupeleka wataalam.kama nchi kwa sasa imeimarisha mifumo mbalimbali ya kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza.
Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii, Dkt Seif Rashid (kushoto), akibadilishana mawazo na katibu mkuu ,Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii,Dkt.Donnan Mmbando (katikati), Balozi wa Tanzania nchini Uswisi, mheshimiwa balozi Modest Mero (mwenye tai nyekundu) na mwambata wa sekta ya Afya katika ubalozi wa Tanzania nchini Geneva Dkt.Catherine Sanga (kulia).
No comments:
Post a Comment