Advertisements

Wednesday, May 20, 2015

UJUMBE WA LEO "KIONGOZI BORA NI YUPI?" | MWL. JK NYERERE

4 comments:

Anonymous said...

Inabidi tufike mahali tumuhukumu Nyerere kwa utawala wake wa kifalme kwa miaka 24 uliotuachia maradhi, ujinga na umasikini wa kupitukia...iwaje anakua mtu wakutueleza kiongozi bora? Nyerere hakukosoleka na kila aliejaribu kumkosoa tunajua kilichompata:( Tuache unafki tuwe wakweli huyu mzee hakuwa kiongozi bora.

Anonymous said...

Tumshukuru Nyerere katuachia nchi yenye amani na maelfu kwa maelfu walisomeshwa BURE bila ya kujali kabila au dini!!!. Watu walisomeshwa kutoka shule ya msingi hadi chuo kikuu BURE!!! WEWE HEBU ANGALIA JINSI MAJIRANI ZETU WOTE WANAVYOHANGAIKA KUITAFUTA AMANI!!! Kwa mfano angalia Kenya,Burundi,Rwanda,Somalia,Congo-DRC,Uganda. etc ..tusifanye mchezo na mambo haya na kuleta USHABIKI USHABIKI usio na msingi wowote.

Huwezi kumlaumu mzee Nyerere mpaka sasa hivi wakati kuna wezi kibao serikalini na kila siku wanaiba na wanaleta udini udini halafu lawama apewe Nyerere.Amka ndugu yangu!!

Anonymous said...

You are wrong. Soma EIU miaka ya Nyerere ndiyo utajiwa kama unayosema si kweli. Wakati wa Nyerere, Healthcare system ya Tanzania was one of the best in the world. Literacy rate was in the high nineties. Of course, we were poor and yes, we are still poor but we did not have as much madeni as now.

Hawa viongozi wako akina Lowassa siyo viongozi bora lkn hawaingii kwa Nyerere.

Anonymous said...

umenena ukweli anonymous wa 7a:36,lakini bahati mbaya ukweli mwengine umeubania. kwanza hakuna binaadam mkamilifu. kwa hiyo Nyerere kama binaadam wengine ana mazuri na mapungufu yake. Nina wasiwasi umeogopa kutaja mazuri yake ili yasije kuyazidi yale mabaya. Nyerere aliamua kuondoka madarakani na ukweli usiopingika angeweza kama anataka angekaa hata miaka 50, kitendo chake cha kungatuka ni cha kishujaa maana viongozi wengi wa kiafrika wanakaa hadi kuuawa au kupinduliwa. Nyerere kaiacha nchi ina umaskini sana lakina ina amani sana. Nyerere hakujilimbikizia mali za kuiibia serikali wala kunyakua ardhi kwa familia yake. Tanzania imebaki haina udini wala ukabila. nataka nikufahamishe ndugu yangu suala la kuondoa umaskini na kuleta maendeleo si la kiongozi peke yake ni ka wananchi wote. tanzania ilikosea na sera zake za ujamaa lakini sasa marekebisho yamefanyika watu wana uhuru zaidi kufanya shughuli za kiuchumi na kuondoa umaskini. Tatizo watu hawajui cha kufanya and in some cases wavivu mno. rafiki yangu mmoja mmarekani hapa US alikwenda vijijini Tanzania kufanya research ya umaskini aliporudi aliniambia 80% ya umaskini wa watanzania unatokana na uvivu. alinambia alipatwa na kiwewe alipoiona ardhi na rasilimali za Tanzania. Nyerere aliwahi kusema uchumi mnao lakini mnaukalia na watu hawakumfahamu kwani watu walianza kupekua matako yao kuutafuta. jamani watanzania tuamke tujiimarishe tusisubiri Rais wala mbunge wala waziri atuletee riziki, tujitume zaidi kiakili na kiwiliwili. nawalaumu viongozi labda hawajawaelimisha wananchi wao maana halisi ya kujitawala. imagine uko na familia yako, you have to make sure you bring food to the table si kusema mbunge ataleta. Jamani Tanzania imebarikiwa sana na kila kitu all resources tumshukuru Mola kwa hilo na pia tuwashukuru viongozi wetu pamoja na mapungufu yao hawajafanya uharibifu wa kupindukia. Mungu ibariki Tanzania