Advertisements

Thursday, May 21, 2015

WANAFUNZI UDOM, DUCE WAGOMA, MADAI NI KAMA YALE YA WENZAO WA UDSM. WANADAI MIKOPO ITOLEWE

WANAFUNZI wa vyuo vikuu vya UDOMA, Mkoani Dodoma ni kile cha DUCE jijini Dar es Salaam, waliamua kuacha masomo na kugoma kushinikiza bodi ya mikopo kulipa mikopo yao. Mgomo huo unakuja siku mbili tu baada ya wenzao wa UDSM kugoma kwa madai kama hayo na hatimaye siku iliyofuatia wakalipwa. Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alilazimika kumtuma naibu waziri wa Afya Steven Kebwe na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa ili kutuliza "mzuka" wa wanafunzi ambapo baadhi yao walilia kwa uchunghu kama Eva Joseph, ambaye naibu waziri alilazimika kufanya kazi ya ziada kumtuliza na kumbebeleza. Pichani juu ni wanafunbzi hao wa UDOM, wakionyesha bango (soma mwenyewe)
Kebwe akimfariji Eva
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa akihutubia wanafunzi hao ambao walikuwa watulivu wakati wote wa mgomo

Picha zote na K-VIS Blog

No comments: