ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 21, 2015

FLAVIANA MATATA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUMBUKUMBU YA WALIOFARIKI MV BUKOBA

Flaviana Matata akiongea neno.Sheikh akiomba dua maalum kwa ajili ya kuwakumbuka marehemu wa ajali ya meli ya MV. Bukoba....wakipiga picha ya pamoja kwenye kaburi....wakipiga picha ya ukumbusho.

Na Johnson James, Mwanza

ALFAJIRI ya Mei 21 mwaka 1996 – siku kama ya leo -- ni tarehe ambayo Tanzania ilipatwa na msiba mzito ambapo zaidi ya watu 600 walifariki baada ya meli ya MV Bukoba iliyokuwa ikifanya safari zake kutoka mjini Bukoba kwenda jijini Mwanza kuzama katika Ziwa Victoria ambalo liko katika eneo la nchi za Kenya, Uganda na Tanzania.

Mwanamitindo maarufu nchini na duniani, Flaviana Matata, wakati wa msiba huo alikuwa na umri wa miaka minane, alikuwa mmoja wa waombolezaji waliofika kwenye misa maalumu ya kuwaombea marehemu waliofariki katika ajali hiyo alimpoteza mama yake mzazi meli hiyo ilipozama maeneo ya Bwiru jijini Mwanza ikiwa na jumla ya abiria wapatao 800.

Katika misa iliyofanyika kwenye kanisa Katoliki huko Nyakahoja jijini Mwanza, mwana mitindo huyo wa kimataifa amesema: “Leo ni siku ambayo sitaisahau kwani ni siku ambayo mama yangu mzazi alifariki kwa kuzama majini na meli ya MV Bukoba katika Ziwa Victoria hivyo niungane na wenzangu waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo ambao ilitwaa maisha ya Watanzania wengi.”

Aidha, katika misa hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, wasanii na vikundi mbalimbali kama Zalendo na Bongo Ride ambao wamewasha mishumaa kwenye makaburi ya marehemu yaliyoko kitongoji cha Igoma jijini Mwanza.

Matata amesema kuwa anaiomba serikali kuhakikisha kuwa vyombo vyote vya majini vinakuwa salama ili kudhibiti ajali za majini ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara.


Flaviana aliongozana na dada yake, Grace Matata, na mshindi wa Big Brother Africa, Sultan Idriss, ambaye alikuwa kivutio cha wengi katika kumbukumbu hiyo.
CREDIT:GPL

No comments: