Advertisements

Wednesday, May 20, 2015

ZIJUE SABABU ZA WANAUME KUCHEPUKA!-2


NI matumaini yangu wapenzi wasomaji wa safu hii mko poa. Leo tunamalizia vipengele vilivyosalia wiki iliyopita, ungana nami.

6.Karaha
Hili pia ni tatizo la wanawake ambalo hawapendi kulikubali. Karaha nyumbani dhidi ya mwanaume huweza kumfanya ajisikie kuhitaji faraja nje ya nyumba. Na wanawake wengi wakimuona mwanaume yupo peke yake baa, hujua kuwa atakuwa amekimbia maudhi ya mkewe na anahitaji faraja.

7.Huruma ya wanawake
Hili nalo ni tatizo linalotumiwa vibaya na wanaume. Wanawake wengi wana huruma na ni wepesi wa kusamehe makosa ya wenza wao. Hii hutokana ama na woga wa maisha peke yao, au kutotaka mambo yao kutoka nje, hivyo huwasamehe haraka wanaume wao hata kwenye makosa ya wazi. Hili huwafanya wanaume kutojali na kurudia tena makosa yao.

8.Kazi na maumbile
Maumbile ya wanaume yako katika namna ambayo ni vigumu sana kwao kuvumilia kwa muda mrefu bila kuhitaji wanawake, hivyo kama wakiwa mbali na nyumbani, hujikuta wakitamani tendo la ndoa.

9.Uhuru uliopitiliza
Kutokana na kazi, wanaume wengi huwa huru kwenye familia zao, kwa kuondoka asubuhi na kurudi usiku mwingi. Hii huwafanya kuweza kufanya lolote wakati wowote bila kuwa na hofu. Ni rahisi kwao kujenga uhusiano na wanawake wa barabarani au hata kazini kwake.

10. Ushawishi wa wanawake
Ingawa kiasili wanaume ni watu wa kutongoza, lakini wapo wanawake ambao huifanya kazi hiyo kwa ajili ya kutaka fedha au kuvuruga uhusiano kwa makusudi. Hutumia mbinu mbalimbali na wanaume hujikuta wameingia mtegoni bila kujua.

GPL

No comments: