ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 30, 2015

ALIYEKUWA MHARIRI WA KAMPUNI YA MWANAHALISI, EDSON KAMUKARA KIJIJINI AZIKWA BUKOBA


Na Faustine Ruta, Bukoba.
Mwili wa aliyekuwa Mhariri wa Kampuni ya Mwanahalisi, Edson Salvatory Kamukara aliyefariki alhamisi ya wiki iliyopita jijini Dar es Salaam umezikwa leo Nyumbani kwao Muleba mkoani Kagera katika Kijiji cha Ihangiro kitongoji cha Bukujungu na kuagwa na mamia ya waombolezaji.Marehemu Edson alizaliwa 27,03.1980 na kufariki wiki iliyopita juni 25, 2015 na amezikwa jana Jumatatu juni 29, 2015. Marehemu walizaliwa Mapacha na ameacha Pacha mwenzake Edda na  ameacha Mtoto wake anayeitwa Edgar.

Viongozi Dini wakiongoza ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu

Pacha wa Marehemu Edson(kushoto) Dada Edda na Kulia ni Dada yao Jeniffer kwenye masikitiko makubwa ya Kuondokewa na Ndugu yao.Katikati ni Dada Joyce akiwa na baadhi ya WanafamiliaMkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea(kulia) akifafanua jambo na mhariri Bw. Ansbert Ngurumo kupitia Gazeti la Tanzania Daima. Picha na Faustine Ruta.
Sehemu ya Wanakwaya wakiendelea kuimba nyimbo Pacha wa Marehemu(kushoto) kwa machungu akiangalia Picha ya Ndugu yake wakati wa Kumuaga kuelekea nyumba yake ya Milele leo jumatatu juni 29, 2015. Picha na Faustine RutaViongozi wa Dini wakitoa salaam zao za mwisho
Dada  wa marehemu Edson Salvatory Kamukara akitoa heshima za mwisho leo jumatatu jioni wakati wa kumuaga.
KWA PICHA ZAIDI SOMA HAPA CHINI
Heshima za MwishoKulia ni Mkurugenzi  wa Radio Kasibante Fm 88.5 nae alikuwepo na hapa akitoa salaam zake za mwisho
Dada yake mkubwa na marehemu Joyce akisoma kwa ufupi historia ya Marehemu Mdogo wake Edson Salvatory Kamukara, Picha na Faustine Ruta
Mwandishi wa TBC Charles Mwebeya akitoa neno
Mwandishi mkongwe na mhariri Bw. Ansbert Ngurumo kupitia Gazeti la Tanzania Daima akitoa neno kuhusu msiba huo wa Mhariri Marehemu Edson S. Kamukara leo wakati wa Kumuaga rasmi Kijijini kwao Muleba kusini.
Umati mkubwa wa Watu walijitokeza kumuaga
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea akitoa neno kuhusu Msiba huo wa Kijana aliyekuwa Mpiganaji kupitia Kampuni hiyo. Kubenea ameweka wazi kuwa Mtoto aliyeachwa na Marehemu kampuni yake itaendelea kuwa karibu nae kimsaada zaidi.
Mwandishi wa TBC Charles Mwebeya akitoa neno kwa Niaba ya waandishi wa Habari Kagera waliojumuika pamoja katika sehemu hiyo kuuaga mwili wa mwenzao Edson Salvatory Kamukara, Picha na Faustine Ruta
Wakati huo huo Mama Mzazi wa Marehemu Edson hakuweza kushiriki alibaki ndani chumbani kwa sababu ya Ugonjwa alionao/ Mlemavu wa Viungo.
Waandishi wa habari Kagera wamejumuika Kuubeba mwili wa Marehemu Edson kuelekea kaburini
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwanahalisi, Said Kubenea akiwa ni moja ya walioubeba Mwili wa Edson kuelekea kaburini.Pacha wa Marehemu akisikitika kuondokewa na mwenzie waliozaliwa pamojaDada wa marehemu Edson akiweka mchanga katika kaburi la aliyekuwa Mhariri wa Kampuni ya Mwanahalisi, Edson Salvatory Kamukara. Picha na Faustine Ruta
Edda Pacha wa Marehemu akiwa kwenye huzuni kubwa

No comments: