Advertisements

Monday, June 29, 2015

FUTARI NYUMBANI KWA MHE, BALOZI RAMADHANI MUOMBWA MWINYI NEW ROCHELLE. NY


Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa New York, Mhe.Balozi Ramadhani Mwinyi pamoja na mama mwenye nyumba wake wakiwa na tabasamu la bashasha baada ya Iftar nyumbani kwao New Rochelle. NY. Mama mwenye nyumba wa balozi pamoja na mume wake waliwakaribisha Watanzania wa jumuiya ya New York nyumbani kwao na kufuturu nao pamoja.

Akina mama wa jumuiya ya Watanzania wa New York wakijiandalia chakula.

Akina mama walikuja na familia zao kama unavyoona kwenye ukodak huu wa Vijimambo.

Mh. Balozi Mwinyi pamoja na mama mwenye nyumba wake wameandaa utaratibu huu wa kufuturu pamoja na wanajumuiya kila wiki endi ndani ya mfungo huu wa Ramadhani.

Akina baba nao wakijiandalia chakula kama unavyoona kwenye ukodak huu hapa mbele yako.

Kama kawaida yake Mhe. Balozi akitoa shukrani mbele ya wageni wake kwa kuitikia mwaliko wake na kujumuika nae kwa Iftar nyumbani kwake.

Kwa picha zaidi nenda soma zaidi.


3 comments:

Anonymous said...

asante sana Mh.Balozi mwenyezi mungu akulipe wewe na familia yako juu yahili,nadhani utakua ndio balozi wa kwanza kufanya hivi hapa New York.,.safi sana

Anonymous said...

kumekucha kwa mungu kwema.mashallah wafungaji wote wamefutarishwa si haba Alhamdulillah.baraka fikh ya balozi wa ny

Anonymous said...

Mhe. Balozi umefanya vizuri sana kuandaa hii futari ya pamoja. Tungependa kujua anwani ya eneo husika maana wengine tungependa kuhudhuria. Asante