ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 18, 2015

Kauli ya LOWASSA Yaleta Gumzo 'Maskini Akienda IKULU Ataiba si Ndio? Tajiri Akienda Ikulu Atawapa watu Mbinu za Utajiri'


Kweli au si kweli? Maskini akienda IKULU ataiba si ndio? Tajiri akienda Ikulu atawapa watu mbinu za utajiri....ama, maskini akienda ataongoza kwa kuelewa matatizo ya wananchi wake na kuwapa kipaumbele...na tajiri yeye hatajali kundi la maskini wanahitaji nini maana hajui umaskini unafananaje?? Vyovyote vile!! Bado tunasikiliza na kupima sera za wagombea wote...

15 comments:

Anicetus said...

Hapa Marekani,Danel Trupn ni tahdiri sana laking watu walinchagu Obama ambaye alikuwa mtoto wa maskini na msahara wake ni wa kawaida.

Bwana Lowassa hajaweza kueleza kwanini na atanafanya mabadiko gani atakapokuwa raisi wa jamhuir ya Tanzania. Raisi Mh. Mwalinu Nyerere alikuwa maskini lakini alileta mabadiliko nchini.

Anonymous said...

Bwana Edward Lowassa, ni mbinu zipi za utajiri wa kuiba mali ya umma utakazowapa wabongo? Labda utataka kuwafundisha wote wawe wezi au wasanii. Ni kweli kama alivyosema Anicetus, bado hujawaeleza waTZ utaletaje mabadiliko. Ila kumbuka kuwa wabongo wote wanafahamu utajiri wako sio wa ubunifu, ila ni wa wizi wa mali ya umma hii ni pamoja na Richmond. Vile vile ujue kuwa hao mashabiki wote wanaokudanganya ni kwa sababu wanalipwa hivyo vijisenti vya ufisadi ambazo huzitolea jasho. Na utachanyikiwa sana usipoteuliwa, hata kama ukiteuliwa na CCM, ujue huna uwezo wowote wa shindana na UKAWA. Wataweka hadhrani yale mambo yaliyotokea 2008 wakati wa sakata la Richmond. Ungejua kuwa unatakiwa kugombea urais mwaka huu, ungekataa kujiuzuru wakati ule. " Chama kwanza rafiki / mtu baadae".

Anonymous said...

Lowasa akomee kimawazo, kwani Marehemu Rais Nyerere hakuwa tajiri, lakini alihakikisha masilahi ya watanzania yanakuzwa

Anonymous said...

Utajiri sio kikwazo cha kuwa Raisi bora, bali ubadhilifu,uhujumu wa mali ya uma ndio tatizo. Idadi kubwa ya wa naomba ridhaa ya kuiongoza Marekani sio watu hohehahe lakini tofauti na sisi USA huwezi kuwa corrupt ukapenya kupata uongozi,na hata ukipita kwa bahati ya ajabu utaishia kuwa impeached tu..kwetu ni vituko tu.baadhi ya waomba nia walilazima kuachia nyadhifa zao kwa kuhusiwa na kashfa za corruption muda si mrefu,leo ni safi na wamequalify kuwa commander in chief. Hii ndio Tanzania.

Anonymous said...

Natamani watanzania wote wangewaza kama nyinyi.Kwani kuondoa umaskini mpaka aingie Ikulu.Miaka yote aliyokuwa kwenye madaraka mbona hajatuondolea umaskini??Tajiri hashughuliki na siasa.Tulia kula utajiri wako uliotuibia watanzania kwa kiasi kikubwa.Acha kumtukana Hayati baba wa Taifa......hakuwa tajiri ila aliitetea nchi na kulinda maliasili zetu.

Anonymous said...

Kwa miaka kadhaa nimekuwa na kigugumizi cha kuukana uraia wa Tanzania, lakini safari hii huenda CCM ikanirahisishia sana uamuzi wangu. Siku Lowasa atakapochaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania, ndiyo siku ambayo nitaukana rasmi uraia wangu wa Tanzania, kwa sababu huo utakuwa ni ushahidi kwamba Tanzania ina ugonjwa wa kutojitambua.

Anonymous said...

Mmeshindwa kumuelewa alichosema Lowassa, amesema kuna wagombea wengine wanajisema kuwa ni maskini ili wawadanganye wananchi na wapate huruma ya watu. Kila mtu ana haki ya kugombea tukianza huo mchezo wa kusema mimi maskini ndiyo napaswa kwenda Ikulu nitakuwa nakosea, hata matajiri ni raia na wana sehemu yao katika jamii.

Anonymous said...

Nikikumbuka uongozi wa Lowasa akiwa waziri mkuu nacheka mwenyewe.Kuna kupindi mheshimiwa alikwenda Thailand kwa gharama za serikali kujifunza jinsi ya kutengeneza mvua "artifical rain"..

Unknown said...

Duh huyo aliyesema kukana Tz, basi angeanza sasa. Hata kuwa na passport ya ki marekani nilazima urudishe ya Tz. Sasa kama huyu ni raia wa USA basi alisha ukana utanzania hata kabla ya Lowasa kutaka kuwa rais. Na usishangae watu wengi wanaosema hovyo waliuza viwanja vya baba zao kusudi waje marekani.....kama ulitoka kwenye udongo,basi utarudi udongoni tu. Ninani anayeweza kutaja kihasi gani cha pesa kilicho ibwa serikalini na Lowasa..? Si mtetei Lowasa ila Watanzania tuache majungu.

Anonymous said...

Obama hakuchaguliwa kwa sababu ni maskini, alichaguliwa kwa sababu nyingi kubwa ikiwa alikuwa muongeaji mzuri sana kwenye Democratic Caucasus iliyopita ya wakati wa John Kerry hivyo 'speech' yake ilimjenga sana akawa 'rising star' pili watu walishachoka na 'prolonged war' ya Iraq na Afghanistan , hivyo wengi waliona ingekuwa vyema wampate mtu aliye jasiri kumaliza vita hivyo (vita ambavyo havishindiki, angalau wanajeshi wengi warudi nyumbani) Obama alikuwa ana nafasi kubwa kwa sababu alivyokuwa senator wa Illinois alipinga vita vya Iraq (as opposed to Mrs. Clinton and others) hiyo sababu ilimpa edge, Obama hakuwa masikini, kama senator alikuwa anayo uhakika wa kazi na flow ya pesa nzuri tu....hata kampeni yake ilikuwa na pesa nyingi ( USA ushindi wa mgombea unategemea na pesa kiasi gani unazo kwa kampeni). Nyerere hakuwa maskini (unless unayo definition tofauti ya umaskini) kwa sababu aikuwa ana kazi tayari na pia alikuwa na eimu ambayo ni asset kubwa ukizingatia wasomi waikuwa wachache sana hivyo alikuwa anayo mshahara wa kutosha. Suala la Lowassa mmelikuza katika njia tofauti.....Lowassa hakusema tajiri ndiyo anatakiwa aingie ikulu ila alisema kuwa "Kuna watu wanaona umaskini ndiyo qualifications ya kupata urais" watu hao wanaojifanya maskini wamekaa miaka mingi kwenye hii hii serikali. Ina maana walikuwa wanafanya kazi kama volunteers, hao wanaojifanya maskini hadi leo wapo serikalini na kila mmoja anajua jinsi serikali yetu ilivyo fisadi.....lakini wanapiga tu kelele lakini hawajiuzulu ina maana wanakubaliana na yote yanayofanywa na serikali. Ni nafuu Lowassa aliyejiuzulu ingawa halikuwa kosa lake, lilikuwa kosa la baraza zima la mawaziri na rais Kikwete.

Anonymous said...

Sisi hatuna tatizo na utajiri wa mtu, bali tunaangalia mchakato ambao huyo mtu ameutumia kupata huo utajiri wake. End does not justify means, but means can justify end. Sote tunajua utajiri wa Lowasa haukupatikana kihalali. Kama alishindwa kulinda maslahi yetu alipokuwa kwenye ngazi ya waziri, hatuna sababu ya kuamini kwamba ataweka mbele maslahi yetu atakapokuwa kwenye ngazi ya Rais wa Jamhuri ya Tanzania. Political insulation atakayokuwa nayo kama Kiongozi Mkuu wa Taifa ndiyo itamfanya ayaumize maslahi yetu zaidi ya alivyoyaumiza hapo awali. Chonde chonde, wapiga kura wenye dhamana, tuepusheni na hili janga!

Anonymous said...

Wewe Joel acha njaa zako, umepewa vijisenti ndio unapiga ngebe. Ukitaka kujua ni kiasi gani cha pesa kilichoibwa Serikalini na Lowassa, unatakiwa uwasiliane na mtunza fedha wake Rostam Aziz, au Karamagi, au Msabaha, au Chenge watakupa hesabu ya haraka haraka. Ukitaka kupata hicho kiasi kwa taratibu itabidi usubili jina lake lipitishwe na CCM, hapo ndipo UKAWA watakupa taarifa kamili.

Anonymous said...

Kwanini Lowasa asijisafishe mwenyewe kutokana na kashfa zinazomkabili ili tutambue kuwa yote yanayozungumzwa against him ni majungu?

Unknown said...

Ninachowezakusema ni kwamba, kila binadamu ana natatizo yake. Hata huko ninakotoka.... watu wakiona umetajirika basi wataanza kusema yakwao. Nina imani hata nyinyi mkipewa nafasi kidogo tu,mtafanya yaleyale wanayofanya viongozi wetu. Swala la nani apeperushe bendera ya ccm tuwaachieni ccm wenyewe na hasa watanzania.
Kama ccm watamchagua basi,acha wananchi wahamue wenyewe. Napenda mabadiriko,lakini sipendi majungu au kashifa. Na kama mungu amepanga Lowasa kuwa rais wa Tanzania,basi
itakuwa hivyo. Alichokipanga mungu,mwanadamu hawezi kukitengua. ......Tanzania hakuna upinzani au tuseme vyama vingi. Kuna wapiga debe wa chama tawala tu. Wewe uliona wapi kiongozi anapata kura 900 kati ya millioni 10,000,000 na bado anaendelea kuomba kuwa rais wanchi.... asanteni wote mnaochangia mawazo ya kumtafuta mgombea saaaafi.

Anonymous said...

Ila siku nyingine hata kama umepewa hela ya rushwa Joel usijaribu kuropokaropoka. Mwaka 2008, jamaa yako aliyekukatia alilia bungeni na kuomba kujiuzuru ili mambo Richmond yaishe. Ililushwa live kwenye Tv kadhaa kumbukumbu zote bado zipo, ambazo zitawekwa wazi muda ukifika. Sasa wewe unapiga kelele za nini? Kosa kushikishwa? Watanzania wanaendelea kumuomba MUNGU, NAYE atatoa kiongozi aliyemuandaa.