Mbuzi wakitimua mbio ili kumpata mshindi wa shindano lililopewa jina la ‘The Kilitime Stakes’ lililodhaminiwa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakati wa mashindano ya mwaka huu ya Mbio za Mbuzi jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mbuzi wakishindana katika mbio za ‘the Toyota value+ grand national’ wakati wa mashindano ya mwaka huu ya Mbio za Mbuzi za hisani jijini Dar es Salaam. Mbio hizo zilikuwa na madhumuni ya kukusanya fedha ili kusaidia watu wenye mahitaji.
Mwenyekiti wa kamati ya Mbio za Mbuzi, Bi. Karen Stanley akihojiwa na waandishi wa habari wakati wa mashindano hayo.
Washiriki wa shindano la mavazi wakijinadi ili kujaribu bahati zao. Mbio za mwaka huu zilikuwa na kauli mbiu ya ‘Bollywood’ambayo ni kiwanda cha filamu cha India, hivyo washiriki wengi walivaa mavazi yenye asili ya watu wa nchi hiyo.
Mbuzi wakimalizia mbio zilizoitwa ‘The CBA Sparkers’ wakati wa mashindano hayo zilizodhaminiwa na benki ya CBA.
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Roberto Jarrin (wa tatu kulia) akikabidhi cheti kwa mwakilishi wa asasi ya KidzCare, Diana Alex wakati wa mashindano ya mwaka huu ya Mbio za Mbuzi za hisani jijini Dar es Salaam. TBL ilikuwa wadhamini wa mbio hizo zenye madhumuni ya kukusanya fedha ili kusaidia watu wenye mahitaji. Wengine kutoka kulia ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Kushilla Thomas.
No comments:
Post a Comment