ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 9, 2015

MBWA DOMO BAYA LAWAMANI KWA KUMTOROSHA BUNDI WA KAMANDA

Jumamosi ya 6 Juni 2015 inasemekana haikuwa nzuri katika kambi ya FFU -ughaibuni baada ya msimu wa joto kuanza nchini ujerumani ,kikosi maalumu cha kuangalia wanyama kiliungana na Kamanda ras Makunja kumsaka Bundi wa mkuu
huyo wa Ngoma Africa Band,Bundi maarufu kwa jina la udi udi alichomoka katika
banda maalumu katika makao ya Ras Makunja marufu kama himaya ya Anunnaki Alien, Kutoroka kwa Bundi huyo kumesababishwa na mbwa wa kamanda aitwae Kopro Dogi Domobaya, mbwa huyo anashutumiwa kwa kuwa mzembe na kuupiga kikumbo mlango wa banda la Bundi na kumfanya bundi kutoroka ,kamanda Ras Makunja aliwambia kikosi cha kuangalia wanyama kuwa "huyu mbwa si mlinzi
mzuri siku hizi amekuwa na utoto sana ! mbwa huyu tangu ampewe zawadi ya mpira watoto wa jirani yeye kazi yake ni kucheza na mpira mpaka kavunja banda la Bundi" Ras Makunja akilalamika na kudai kuwa huyu mbwa akiendelea na uzembe nitamfuta kazi,Pia inasemekana midudu hiyo imetengewa eneo maalumu katika himaya ya FFU-ughaibuni, Bundi huyo baadaye alirudi mwenyewe baada ya kutoweka kwa masaa kadha.

No comments: