ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 3, 2015

TAMKO KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA BAJETI YA AFYA, KASMA YA UZAZI WA MPANGO

 Tamko hili linatokana na shughuli zinazoendelea za shirika hili za ushawishi na utetezi kuitaka serikali iongeze kiwango cha fedha kinachoelekezwa katika kasma ya uzazi wa mpango, chini ya bajeti ya afya.

Pamoja na tamko hili, UNA Tanzania iliendesha mafunzo na mjadala wa siku moja na waheshimiwa wabunge siku ya Jumapili, tarehe 31 Mei 2015, Dodoma. Wajumbe katika mjadala huo walitoka katika Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, pamoja na Klabu ya Wabunge ya Uzazi wa Mpango. Katika mjadala huo, wabunge walipata kusikiliza mawasilisho (presentations) kutoka kwa wataalamu watatu juu ya;
  1. Umuhimu wa Uzazi wa Mpango, na Mwenendo na Mahitaji ya Kifedha katika kufikisha huduma kwa Watanzania,
  2. Hali, Mahitaji ya Mafunzo na Vipaumbele katika kuhakikisha uwepo wa Watoa huduma za Uzazi wa Mpango,
  3. Hali na Upatikanaji wa Njia za Uzazi wa Mpango.
Tumeambatanisha pia picha chache kutoka katika mjadala huo. Tutashukuru kama sehemu au tamko hili kwa ujumla, au swala la uzazi wa mpango litapata nafasi katika chombo chako cha habari wakati tathmini ya Bajeti ya Wizara ya Afya ikiendelea.

Tunashukuru sana kwa ushirikiano wako. Tamko kwa lugha ya kiingereza litasambazwa kabla ya tarehe 04/06/2015



No comments: