Makamu wa Rais wa Kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Acacia,Deo
Mwanyika akizungumza wakati wa hafla fupi ya mapokezi kwa timu
iliyoshiriki kupanda Mlima Kilimanjro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa
ajili ya shule za Msingi.
Mkuu wa wilaya ya Tarime,Glorious Luoga akizungumza katika hafla hiyo.
Afisa Mtendaji mkuu wa Kampuni ya Acacia ,Brad Gordon akikabidhi
mfano wa hundi ya kiasi cha Shilingi Milioni 800,000,000 kwa mkuu wa
wilaya ya Tarime ,Glorious Luoga ,zilizochangwa kupitia mpango wa
CanEducate kwa ajili ya kusaidia elimu
Tanzania.
Mkuu wa wilaya ya Tarime,Glorious Luoga akiwa amenyanyua juu mfano wa Hundi.
Timu ya watu 21 ya wafanyakazi ,Ndugu na Marafiki wa Kampuni ya
kuchimba dhahabu ya Acacia wakishuka kutoka mlima Kilimanjaro ambako
walipanda kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia
elimu.
Afisa Mtendaji mkuu wa Kampuni ya uchimbaji wa Dhahabu ya Acacia,Brad
Gordon akiwa na Meneja wa Ustawi wa kampuni Asa Mwaipopo wakifurahia
mara baada ya kushuka toka kaika kilele cha Uhuru ambako watu 19 kati ya
21 ndio walifanikiwa kufika
kileleni.
Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma wa kampuni
ya kuchimba Dhahabu ya Acacia,Necta P Foya akishangilia wakati akishuka
toka mlima Kilimanjaro.
Timu ya watu 21 iliyopanda Mlima Kilimanjaro kutoka kampuni ya
Kuchimba Dhabu ya Acacia wakiwa katika Uniform maalumu wakielekea lango
la kutokea katika mlima la Mweka huku wakiimba nyimbo mbalimbali.
Mkuu wa wilaya ya Tarime ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika
mapokezi ya timu ya watu 21 iliyopanda mlima Kilimanjaro,G;orious Luoga
(wa tatu toka kushoto) akiimba na wapandaji
hao.
Wapandaji wakiimba mara baada ya kufika katika lango la Mweka,hapa
wakiongozwa nyimbo mbalimbali na mmoja wa asakari wa Hifadhi ya taifa ya
Mlima Kiliamanjaro.
Afisa mtendaji mkuu wa Kampuni ya kuchimba Dhahabu ,Brad Gordon
akifurahia na wafanyakazi wa kampuni hiyo,Meneja wa kitengo cha
Mawasiliano na Uhusiano wa Umma,Necta Foya na Fredrick Njoka
Timu ya watu 21 waliopanda mlima Kilimanjaro,wakiwa katika picha ya
Pamoja katika lango la Mweka mara baada ya kushuka toka Kilele cha
Uhuru.
Baadhi ya washiriki wa zoezi hilo la kupanda Mlima Kilimanjaro
Mkuu wa Wilaya ya Tarime ,Glorious Luoga akiteta jambo na Afisa
Mtendaji mkuu wa kampuni ya kuchimba Dhahabu ya
Acacia.
Kaimu Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Charles
Ngemba akizungumza wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya timu ya watu 21
wakiwemo wafanyakazi ,Ndugu na marafiki wa kampuni ya kuchimba Dhahabu
ya Acacia
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii
Kanda ya Kaskazini.
1 comment:
Haya makampuni ya madini ndio wezi wakubwa. Wasitudanganye wanachanga fedha za kujenga shule
Post a Comment