ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 30, 2015

SHUKURANI KWA WATANZANIA KUTOKA KWA FAMILIA YA MAGEGE NA JUMUIYA YA WATANZANIA NEW YORK.




Jumuiya ya Watanzania New York,New Jersey,Connecticut na Pennsylvania
kwa pamoja na Magege's Family,Tunatoa shukurani zetu za dhati kwa wote
waliojitokeza kwa namna Moja au nyengine katika kufanikisha mazishi ya
Mpendwa Mzee wetu Alfred Magege.
Kwa pamoja tumefarijika na upendo mliotuonyesha katika Kipindi chote
cha Msiba wa Mzee wetu na
Hatuna cha kuwalipa isipokuwa kukuombeeni dua kwa Mwenyezi Mungu
akuzidishieni Baraka na Daima tuendelee kuwa wamoja katika shida na
raha.

Vile vile Tunatoa Shukurani maalum kwa ofisi za Wawakilishi wetu wa
kudumu Umoja wa Mataifa New York pamoja na Uongozi wa CCM tawi la New
York chini ya Uongozi Thabiti wa Bwana Seif Akida. Ushirikiano wenu
Kwetu ni changamoto na Daima tutauenzi. Ahsanteni Sana.

Bila kuwasahau Boston Tanzanian Community kwa ushirikiano wenu wa
karibu,Bwana Geoffrey Ngullu kutoka Philadelphia kwa usimamizi wako,
 Vijimambo Timu, Dr Temba wa Temba Photo kwa picha
Nzuri,Kinamama waliojitolea kupika pamoja na Pastor Nkarlo Alexander
na Waumini wote wa Victory Seventh-Day Adventist Church. 
Ahsanteni
Sana.

Hajji Khamis
Mwenyekiti
NY Tanzanian Community

Mke wa marehemu mzee Alfred Magege.

Mama na watoto wake , Kwa taswira zaidi nenda soma zaidi






Kwa picha zaidi tembelea

2 comments:

PETRO said...

Umoja ni nguvu

Anonymous said...

kweli kabisa ummoja na nguvu utengano ni dhaifu na samahanini kwa tulioshindwa kuja tusameheyeni sana.lakini tulikuwa pamoja na nyinyi katika kiroho kukuombeyeni.

mdau mount Vernon.
na pole sana pia dr Temba.