ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 30, 2015

UTOLEWAJI WA VIWANJA TANZANIA KWA DIASPORA


Uongozi wa Jumuiya ya DMV unapenda kuwajulisha kuwa Wizara ya Ardhi ikishirikiana na Idara ya Diaspora kwenye wizara ya Mambo ya nchi za Nje; kuwa Wanadiaspora, mnashauriwa,  mnaruhusiwa na mnaweza kuomba Ardhi kwa ajili ya uwekezaji nyumbani Tanzania.

Mnaweza kutuma maombi yenu moja kwa moja kwenda kwa kamishna wa Ardhi kwa kupitia Idara ya Diaspora, Wizara ya Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa kwenye email hii : diaspora@nje.go.tz.

Maombi:

  1. Yaainishe Mkoa au Wilaya ambayo mwombaji anapenda kupatiwa ardhi
  2. Aina ya Matumizi ya Ardhi anoyoomba kama vile Makazi, Biashara, kilimo ama Mifugo.
  3. Kwa Ardhi ya Makazi Mwombaji aeleze aina ya kiwanja anachoomba kama ni “Low Density”, “Medium Density” au “High Density”.


Asanteni
Uongozi

Jumuiya DMV