Mkurugenzi wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu akitoa maelezo kwa mgeni Rasmi Mheshimiwa Samuel Sitta alipotembelea banda la Ofisi ya Makamu wa Rais katika maadhimisho ya wiki ya siku ya mazingira jijini Tanga. Wengine wanaosikiliza ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt Binilith Mahenge (kulia) na Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais-Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan (kulia).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith Mahenge akimkaribisha mgeni Rasmi ili aweze kuzindua maadhimisho ya wiki ya Mazingira duniani katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya siku ya mazingira duniani Mheshimiwa Samuel Sita akihutubia katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
Watanzana wametakiwa kutunza na kuthamini mazingira kwa
sababu ni urithi wa thamani kubwa sana kwa kizazi cha sasa na kijacho. Hayo
yamesemwa na Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya siku ya mazingira Duniani, Mheshimiwa Samuel Sita- Waziri
wa Uchukuzi ambaye alimuwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Mohammed Gharib Bilal.
Akiongea na Wananchi katika viwanja vya Tangamano vilivyopo
katika jiji la Tanga Mheshimiwa Sita amesisitiza juhudi zaidi katika suala zima
la utunzaji wa mazingira na kuwaomba Wazazi kuelemisha watoto wao umuhimu wa
kuthamini mazingira. Aidha amewapa hongera Wananchi na Viongozi wa jiji la
Tanga kwa kutilia mkazo usafi wa mazingira na kufanya jiji hilo kuibuka mshindi
wa tatu katika mashindano ya usafi wa mazingira kitaifa.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi ili kufungua sherehe hizo Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Binilith Mahenge aliesma ni
jukumu la kila mmoja kutunza na
kuhifadhi mazingira hivyo basi kila Mwananchi ajitahidi katika hilo.
Siku ya mazingira duniani hufanyika kila tarehe tano ya
mwezi Juni kila mwaka. Kauli mbiu ya mwaka huu ni Ndoto bilioni saba, dunia
Moja , tumia Rasilimali kwa uangalifu.
Hii ikimaanisha kutumia vema rasilimali zetu ili kutunza vema mazingira yetu.
No comments:
Post a Comment