ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 19, 2015

Wananchi wazidi kumiminika Banda la Mambo ya Nje Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma

Afisa kutoka Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar, Bi. Asiya Hamdani akitoa maelezo kuhusu majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Wananchi waliokuja kutembelea Banda la Wizara lililopo katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni "Utumishi wa Umma katika Bara la Afrika ni Chachu ya Kuwawezesha Wanawake, Kuongeza Ubunifu na Kuboresha Utoaji Huduma Kwa Umma". 
Afisa matukio msaidizi kutoka Taasisi ya APRM, Bi. Praxeda Gasper akitoa maelezo kwa mwananchi aliyetembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Nje. 
Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Thobias Tarimo naye akielezea majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa mmoja wa wananchi waliojitokeza kwenye maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye Banda la Wizara hiyo. 
Mkufunzi wa Chuo cha Diplomasia kilichopo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Desderia Sabuni (wa kwanza Kushoto) naye akiwaelezea wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Mambo ya Nje juu ya Kozi mbalimbali zinazotolewa na Chuo cha Diplomasia pamoja na majukumu ya Wizara kwa ujumla. 
Wananchi wakiendelea kupata huduma kwenye Banda la Mambo ya Nje 

Picha na Reginald Philip

No comments: