Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akiongea na wananchi waliojitokeza kuwasilisha kero zao katika ukumbi wa chuo cha ualimu Mtwara. Alisisitiza kuwa Mkoa wa Mtwara uharakishe kupima ardhi ya wananchi ili kupunguza migogoro ya ardhi.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akionyeshwa na Maafisa waandamizi wa sekta ya ardhi kanda ya Kusini taarifa yenye mpango Mji wa Mtwara(Mtwara Master Plan) unaoendelea kukamilishwa alipozuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara katika ziara yake mkoani humo.
Meneja wa NHC Mkoani Mtwara Bw. Joseph John akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi wa nyumba unaotekelezwa na NHC eneo la shangani Mtwara ambapo alisema kuwa mradi huo utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 4 hadi kukamilika.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akilitaka Shirika la Nyumba kutumia fursa zilizopo Mkoani Mtwara hivi sasa kwa kuongeza ujenzi wa nyumba za makazi na biashara alipotembelea nyumba zinazojengwa na NHC eneo la Shangani Mtwara.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha(AICC) walialikwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi katika ziara yake kiwanda cha saruji cha Dangote ili kujifunza namna ya kuwekeza Mkoani Mtwara. Kituo hicho cha Mikutano kinakusudia kuwekeza Mkoani Mtwara kwa kujenga ukumbi mkubwa wa kimataifa wa mikutano.
Ofisa Ardhi Mteule wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Bw. Michael akijitetea kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi baada ya wananchi kumtuhumu kutowapa huduma kwa haki na kuchelewesha kuwapimia wananchi ardhi yao.
Sehemu ya umati wa wananchi wa Mkoa wa Mtwara wakimsikiliza Waziri Lukuvi aliposikiliza kero zao katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Mtwara.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akipewa taarifa na uongozi wa kiwanda kikubwa cha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara alipopata nafasi ya kutembelea kiwanda hicho ili kuondoa kero zinazomkabili mwekezaji huyo. Kiwanda hicho kitakachoanza uzalishaji mwezi Agosti mwaka huu kina uwezo wa kuzalisha tani 7500 za saruji kwa siku.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Vangimembe Lukuvi akizungumza na watendaji wa sekta ya ardhi na Sekretarieti ya Mkoa wa Mtwara ambapo alisisitiza uadilifu na utendaji haki katika kuhudumia wananchi ili kuondoa migogoro ya ardhi.









No comments:
Post a Comment