ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 9, 2015

ZIARA YA KINANA MULEBA, JANA JUNI 8, 2015

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kata ya Izigo, jimbo la Muleba ya Kaskazinimoani Kagera.
 Wakazi wa Izigo wakiinua ikono juu kama ishara ya kuafiki hoja za Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye amemaliza ziara yake kwenye jimbo la Muleba Kaskazini.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Izigo ambapo aliwaambia kuwa mwaka huu CCM itashinda vizuri kutokana na sera zake nzuri na zinazotekelezeka.


 Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Charles Mwaijage akishiriki kucheza ngoma ya asili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Asbert Ngurumo mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara uliofanyika Izigo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maeezo juu ya mradi wa ufugaji samaki katika kata ya Ruhanga.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi pampu ya maji zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo Mhe. Charles Mwihage kwa ajili ya umwagiliaji ambayo zilitolewa kwa vikundi mbali vya kijasirimali.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Tawi la Kamachumu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Kamachumu ambapo aliwaambia hakuna kitu magendo katika zao la Kahawa ila ni bei tu ya vyama vingi vya ushirika inawanyonya wakulima,alisema vyama vya ushirika vipunguze utitiri wa kodi na kwendana na bei yenye ushindani kwenye soko.
 Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini ambaye pia ni Naibu Waziri Nishati Charles Mwijage (kushoto)akimuongoza Katibu Mkuu wa CCM kucheza ngoma ya asili inayojulikana kwa jina la Bikorwengonzi wakati wa mkutano wa hadhara Kamachumu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Mushabago, Muleba ya Kaskazini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mushabago,Muleba ya Kaskazini.

 Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini Charles Mwijage akihutubia wakazi wa Mushabago ambapo alisisitiza kufanya uchaguzi mzuri wa madiwani wa CCM kwani watasaidia kusukuma utekelezaji wa ilani ya CCM na kurahisisha kuleta maendeleo.
 Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini akionyesha uwezo wa kucheza ngoma ya asili.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangali Kompyuta za shule ya Sekondari ya Nyakatanga zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini Mhe.Charles Mwijage.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimia wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nyakatanga ambapo Mbunge wa Jimbo la Muleba ya Kaskazini alikabidhi kompyuta na kuwasha umeme kwa mara ya kwanza kwenye shule hiyo.
 Mbunge wa Muleba ya Kaskazini na Naibu Waziri Nishati Charles Mwijage akizungumza mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nyakatanga ambapo alikabidhi kompyuta saba kwenye shule hiyo.
 'Umoja ni Nguvu' , Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi wengine wa chama na serikali akishiriki zoezi la kutandanza umeme wa mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Nyakatanga, Muleba Kaskazini.


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Nshamba
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amebeba muwa ambao alipewa zawadi na wakazi wa Nshamba, Muleba ya Kaskazini.
 Wananchi wa Nshamba wakimsikiliza Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Nshamba.
 Mbunge wa Muleaba ya Kusini Profesa Annatibaijuka akihutubia wakazi wa kata ya Nshamba ambapo aliwasisitiza kwa wananchi hao kutunza chanzo cha maji.


No comments: