Advertisements

Tuesday, July 28, 2015

DIDIER DROGBA AJIUNGA NA KLABU YA MONTREAL IMPACT YA CANADA

do
Baada ya kumaliza mkataba wake na Chelsea, mshambuliaji wa Ivory Coast, Didier Drogba amesaini mkataba wa miezi 18 wenye thamani ya dola milioni tatu kwa mwaka na klabu ya Montreal Impact inayoshiriki ligi kuu ya Marekani na Canada, Major League Soccer.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 aliondoka Stamford Bridge baada ya kuichezea timu hiyo mechi 381 na kushinda makombe manne ya Premier League.
Rais wa klabu hiyo yenye makazi yake nchini Canada, Joey Saputo alisema kumchukua mshambuliaji huyo ni kitu kikubwa zaidi kwenye historia ya klabu hiyo.

Jiunge na Bongo5.com sasa

No comments: