Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC),Jaji Mstaafu,Damian Lubuva (katikati) akizungumza na waandishi habari juu
juu ya maendeleo mbalimbali katika kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika leo Makao
Makuu ya NEC jijini Dar es Salaam,Kulia Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar
es Salaam,Kamishina Suleiman Kova na Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji
Uchaguzi,Clothilde Komba.
Kamanda wa polisi wa Kanda Maalumu
ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akizungumza na waandishi habari juu
juu jeshi la polisi lilivyojipanga
katika suala la ulinzi kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika leo Makao Makuu ya
NEC jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakifatilia wa
taarifa ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji Mstaafu Damian Lubuva
leo Makao Makuu ya NEC jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka )
Na Chalila Kibuda
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kuanza kutoa fomu ya urais ,Ubunge
pamoja na Udiwani kesho na kumalizika kwa zoezi la utoaji fomu hizo ni Agasti
21 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji
Mstaafu,Damian Lubuva amesema wakati wa
uchukuaji wa fomu ya urais itatolewa bure lakini wakati wa kurudisha anatakiwa
kuweka dhamana ya Sh.milioni Moja na wadhamini wadhamini 200 katika kila mkoa
na kuwepo kwa mikoa miwili Zanzibar.
Lubuva a amesema kuwa wakati wa
kuchukua fomu viongozi wa vyama vya kisiasa wanatakiwa kuchukua fomu na
kurudisha bila kuwa na kundi kubwa ambalo linaweza kusimamisha shughuli za watu
wengine.
Amesema kwa fomu za ubunge ni
sh.50,000 na udiwani sh.5000 ambapo
wanatakiwa kuchukulia katika ofisi za wilaya na uchukuaji huo lazima uwe wa
kistaarabu katika kuweza watu wengine waendelee na shughuli zao.
Lubuva amesema kuwa wanasiasa wanatakiwa na lugha za kistaarabu katika mikutano yao
katika kujenga demokrasia iliyo ya ukweli.
Hata hivyo amesema kuna baadhi ya
vijana wanauza kadi za tume ya taifa ya uchaguzi na kutaka vyombo vya usalama
kuchunguza pamoja na kuwachukulia hatua watu wanaouza kadi hizo.
Kamanda wa Polis wa Kanda Maalum ya
Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova amesema kuwa uchaguzi unaendana na usalama hivyo jeshi limejipanga katika
ulinzi katika kipindi hiki.
Kova amesema kuwa Jeshi litaendelea
kushirikiana na viongozi wa siasa katika kuleta amani katika kipindi cha
uchaguzi.
1 comment:
Sawa kamanda ila tuache kutupiana mabomu Tanzania sio Iraq wala Afganistan. La msingi pia tuangalizieni wizi wa kura usitokee kwa kengo la kufunga kwa goli la mkono!!
Post a Comment