Advertisements

Monday, July 27, 2015

IKULU YAKANUSHA TAARIFA YA GAZETI LA MWANANCHI LA JULAI 27, 2015


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Gazeti la Mwananchi la leo, Jumatatu, Julai 27, 2015, kwenye ukurasa wake wa 26 limechapisha habari yenye kichwa cha habari, “Marais watano wanaotajwa kuongoza kwa mishahara minono barani Afrika ni hawa hapa”.

Katika habari hiyo ambayo gazeti hilo linadai chanzo chake ni “uchambuzi wa mtandao wa African Review” inadaiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, anashilikia nafasi ya tano miongoni mwa viongozi 38 wa nchi za Afrika wanaolipwa mshahara mnono zaidi.

Gazeti hilo linadai kuwa Rais Kikwete analipwa Dola za Marekani 192,000 kwa mwaka, ikiwa ni malipo ya Dola za Marekani 16,000 kwa mwezi.

Habari hizi siyo za kweli. Ni uongo na uzandiki. Ni uzushi mtupu na ni uzushi wa hatari.


Mshahara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwezi ama kwa mwaka haufikii na hata wala kukaribia kabisa kiwango kinachotajwa na Gazeti la Mwananchi.

Tangu Uhuru, mwaka 1961, Rais wa Tanganyika na baadaye tangu mwaka 1964 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekuwa miongoni mwa viongozi wanaolipwa mishahara ya chini kabisa duniani.

Mshahara wa Rais wa Tanzania kwa mwezi ni wa chini kiasi cha kwamba mshahara wake unazidiwa, tena kwa mbali, na mishahara wanayolipwa baadhi ya watendaji wakuu wa baadhi ya taasisi za umma nchini.

Aidha, ni jambo la kushangaza kwamba Gazeti la Mwananchi, linalochapishwa hapa nchini, linaweza kupata kiasi cha uongo anacholipwa Rais wa Tanzania katika mitandao ya nje badala ya kuuliza rasmi na kupewa majibu sahihi.

Kwa kujiingiza katika uzushi wa kupindua kiasi hiki, Gazeti la Mwananchi haliwezi kuwa na nia nyingine yoyote isipokuwa nia ya kuwachochea wananchi na kuwajengea chuki dhidi ya Serikali yao na Kiongozi wao Mkuu.

Ni matarajio yetu, kuwa Gazeti la Mwananchi litafanya jitihada za makusudi, kama taaluma ya uandishi wa habari inavyoelekeza, kutafuta usahihi wa jambo hili na kuwaambia Watanzania ukweli.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
27 Julai, 2015

5 comments:

Anonymous said...

NYIE WATU WA IKULU MNATAKIWA MUWE NA AIBU WAKATI MWINGINE. SIKATAI KUIPINGA HABARI HII IKIZINGATIWA HIYO NDIYO AJIRA YENU. TATIZO NI KWAMBA MNAPOAMUA KUDISPUTE ANY REPORT, THEN IT IS YOUR JOB TO RESPOND WITH THE ACCURATE INFORMATION AND EVIDENCE. SIO KUJA NA HABARI ZA KITOTO KWAMBA RAIS WA TANZANIA ANALIPWA MSHAHARA MDOGO TANGU WAKATI WA UHURI. KILA MTU ANAJUA MSHAHARA WA MWALIMU ULIKUWA CHINI YA SHS 5000 KAMA SIJAKOSEA NA ULIKUWA PUBLIC. SASA KAMA UNASEMA JK HALIPWI DOLA 16000 KWA MWEZI, THEN HOW MUCH IS HE PAID MONTHLY OR ANNUALLY? YOU DO NOT NEED PHD TO ANSWER THIS. NI MIMI MJENGWA JR.

Anonymous said...

Kama mnakanusha si mtueleze analipwa kiasi gani.Ubabaishaji mwingi serikalini ndio maana chuki inazidi juu yenu.Hii ni kazi ya uma na niwajibu wa serikali kuijulisha jamii.

Anonymous said...

tell us what he gets then. Mwananchi has given us figures, what are your figures Ikulu?

Anonymous said...

Ikulu kama hmuwezi kutoa figures it is better to shut up.

Anonymous said...

Why is this subject so important? A common man does not care very much about the President's or anybody else salary! Tulipomchagua hatukuuliza atapata pesa ngapi, hivyo ni ajabu wapinzani wanalialia kama watoto wadogo. Rais amefanya kazi nzuri kwa Taifa, and if I had the power, ningempa Twice as much.
Mimi ni mdau marekani, Asanteni.